Waziri wa Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Bweni la Wasichana lenye ghorofa 4 linalojengwa kwa thamani ya shilingi Bilioni 2.2 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Misungwi Wilayani Misungwi ,Mkoani Mwanza.
Dkt. Gwajima ameridhishwa na maendeleo yanayofanywa na Chuo hicho, wakati wa ziara yake Wilayani Misungwi ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Bweni la Wanafunzi wa kike tarehe 17 Septemba, 2024 sambamba na kuhamasisha jamii kutokomeza ukatili, ndoa, na mimba za utotoni, na ukatili wa kijinsia pamoja na kuhamasisha Wananchi kujiletea maendeleo katika familia na jamii, ameongeza kuwa Serikali inatambua umuhimu wa Taaluma inayotolewa na Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Misungwi pamoja na mambo mengine Serikali inahakikisha uwepo wa mazingira salama kwa Wasichana na kuwajengea uwezo katika fani ya maendeleo ya jamii na ufundi ili waweze kujimudu na kukuza uchumi binafsi na taifa kwa ujumla.
Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia,Wanawake,na Makundi maalum Mhe. Dkt. Doroth Gwajima akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Johari Samizi wakati wa ziara ya kikazi hivi karibuni katika Chuo cha CDTTI Misungwi
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi (CDTTI) Misungwi Bw. Charles Achuodhu amesema kwamba kwa mwaka wa Fedha 2022/2023 wamefanikiwa kuanzisha mradi wa ujenzi wa Bweni la Wasichana lenye ghorofa 4 na Serikali imeweza kutoa fedha za ujenzi huo ambapo hadi sasa ujenzi upo katika hatua ya msingi uliogharimu kiasi cha shilingi Milioni 300 ambapo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 wanatarajia kupokea kiasi cha Fedha shilingi Milioni 500 kwa ajili ya uendelezaji wa ujenzi wa mradi huo na Jengo litakapokamilika linatarajiwa kuwa na uwezo wa kuchukua Wanafunzi 352 wa jinsia ya kike na kwamba kwa sasa Chuo kina uwezo wa kuwahudumia Wanafunzi 200 tu wa bweni wakati mahitaji yaliyopo kwa sasa ni mabweni ya Wanafunzi takribani 600.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Johari Samizi ameishukuru Serikali na kumpongeza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha za ujenzi wa mradi wa Bweni la Wanafunzi wa kike kutokana na uhaba wa mabweni unaokikabili Chuo hicho sasa kutaleta manufaa makubwa na kuongeza uwepo wa Wanafunzi wengi na kuepuka Wanafunzi wengine kukaa umbali mrefu ambao ungeweza kusababisha matukio au vitendo hatarishi pamoja na kuongeza ufaulu.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.