Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation yatoa misaada ya Kompyuta tano na Vifaa wezeshi 6 vya kujifunzia uzazi salama katika Vituo vitano vya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kwa lengo la kupunguza Vifo vitokanavyo na uzazi kwa akina Mama Wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano.
Akizungumza katika makabidhiano ya msaada wa vifaa hivyo katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi, Afisa Mradi Vijijini Kanda ya Ziwa wa Taasisi ya Benjamin Mkapa, Bi, Scholastica Komba amesema kwamba msaada huo ni pamoja na Kompyuta tano aina ya Dell, Midoli ya Mwanasesele 6 kwa ajili ya kujifunza namna ya uzazi salama kwa akina mama na Baby Natalia 6 ambavyo vifaa hivyo vitasaidia vituo vya Afya hivyo kutoa mafunzo kwa Wauguzi namna ya kumsaidia mtoto aliyezaliwa na shida ya kupumua ambavyo vyote vinathamani ya shilingi Milioni 60.
Bi, Scholastica Komba Afisa Mradi Vijijini Kanda ya Ziwa wa Tasasisi ya Benjamin Mkapa Foundation akimkabidhi Vifaa wezeshi Baby Natalia vya kujifunzia Wauguzi namna ya uzazi salama kwa Wajjawazito na watoto wachanga,kwa lengo la kupunguza Vifo vitokanavyo na uzazi kwa Wajawazito kwa Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt, Zabron Masatu,katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi.
Bi, Scholastica Komba alieleza kuwa lengo ni kusaidia Vituo vya kutolea huduma za Afya kuona matokeo chanya kwa akina mama Wajawazito wakati wa kujifungua pamoja na watoto wanapozaliwa, na vifaa hivyo vitawasidia Wauguzi na Wakunga kupata ujuzi zaidi na uzoefu wa kuwahudumia akina mama Wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua salama na kuhakikisha kwamba Vifo vitonavyo na uzazi kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga vinapungua.
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Dkt, Zabron Masatu alisema kuwa katika Halmashauri ya Misungwi kuna upungufu wa Vitendea kazi ikiwemo na Kompyuta kwa Wataalam wa Sekta ya Afya, hivyo vifaa hivyo vitasaidia sana katika utendaji kazi na kuongeza ufanisi pamoja na kuleta tija katika utoaji wa huduma za matibabu kwa Wagonjwa na hatimaye kupunguza Vifo vya akina mama Wajawazito na watoto wachanga .
Alisema Vifaa hivyo vitapelekwa katika Zahanati ya Mahando, Nyamijundu, Mwaniko, Mwamboku pamoja na Kituo cha Afya Mbarika kwa lengo la kuboresha na kuimarisha utoaji wa huduma za Afya katika maeneo husika.
Bi, Scholastica Komba, Afisa Mradi Vijijini Kanda ya Ziwa, wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa Foundation (kulia) akimkabidhi Kompyuta moja kati ya tano zilizotolewa msaada kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Dkt, Zabron Masatu kwa ajili ya kuwezesha na kuboresha huduma za Afya katika Vituo vitano vya kutolea huduma katika Halmashauri ya Wilaya hii.(kushoto) ni Rose Baluhya Muuguzi katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi akishuhudia makabidhiano hayo hivi karibuni.
Dkt, Zabron Masatu ameishukuru sana taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation kwa kutoa msaada huo katika kipindi hiki cha mahitaji makubwa ya vifaa vya kuwezesha huduma za Afya kuwa bora na kuunga juhudi za Serikali ya awamu ya tano katika kuboresha huduma za Afya hapa nchini.
Mganga Mkuu huyo ameeleza kwamba Vifaa hivyo zikiwemo Kompyuta watahakikisha vinatumika katika uwekaji na utunzaji wa takwimu na kumbukumbu za Wagonjwa na shughuli zote za kitabibu kwenye Vituo hivyo vya kutolea huduma za Afya sambamba na Vifaa vya kujifunza namna ya uzazi salama pamoja na matumizi ya Vifaa vya kujifunzia Wauguzi na Wakunga namna ya kumsaidia kupumua mtoto aliyezaliwa na shida ya kupumua na watahakikisha kwamba vifaa vyote vitatunzwa vizuri na kudumu kwa muda mrefu.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.