Watumishi saba (7) wafukuzwa kazi kutokana na tuhuma za utoro na kukiuka kanuni za utumishi wa umma katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi , Mkoani Mwanza.
Mamauzi hayo yalitolewa na Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi katika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri hiyo jana, ambapo Mwenyekiti wa Halamshauri hiyo Mhe, Kashinje Machibya alieleza kwamba Halmashauari imeridhia uamuzi wa Tume ya uchunguzi ambayo ilipitia mashitaka na kutoa uamuzi wa Watumishi 7 kufukuzwa kazi na wengine wannne kurejesha kazini.
Mhe, Machibya amesema kwamba sababu za kufukuzwa kazi Watumishi hao ni kutokana na kuwa na tuhuma mbalimbali za kiutumishi ikwemo utoro kazini zaidi ya siku tano, udagannyifu na kugushi vyeti vya kidato cha Nne, pamoja na upotevu wa fedha za ushuru wa mapato ya Halmashauri.
Mhe, Machibya ameeleza na kutoa Wito kwa Watumishi wengine kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma na kuwataka kuzingatia kanuni na maadili ya kazi na kwamba wao kama Baraza hawafurahishwi na kitendo cha Mtumishi kuondolewa kazini hivyo waendelee kuwajibika kikamilifu.
Aliongeza kwamba Halmashauri kwa kipindi cha kuishia Julai 2021 imekuwa na usimamizi mzuri katika matumizi ya fedha za Umma ambapo imefanikiwa kuwa na Hati safi katika ukaguzi wa Hesabu za mwaka 2019/2020 zilizofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na kuwapongeza Madiwani wote, viongozi wa Serikali pamoja na Menejimenti kwa ujumla kwa ushirikiano wakati wote.
Kwa mujibu wa taarifa ya Tume ya uchunguzi ilibainisha Watumishi 7 waliofukuzwa kazi ni pamoja na; Alphonce Samula Madukulu ambaye ni Mlinzi kwa kosa la utoro Ernest Msiba Celestine,Daktari wa Kituo cha Afya Misasi kwa kosa la utoro kazini, Wilson S. Alilah aliyekuwa Daktari, kwa mashitaka ya kosa la utoro kazini Hilary W. Mtui ambaye alikuwa Daktari katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi kwa kosa la utoro, Simon Makanga Wilson aliyekuwa Afisa Muuguzi msaidizi katika Zahanati ya Nkinga kwa kosa la utoro kazini , Rozalio Kipondya Aloyce, ambaye ni Mtendaji wa Kijiji cha Seeke kwa kosa la upotevu wa mapato ya ndani shilingi Milioni 3,897,500/=, Bernard Joseph Makungwi, aliyekuwa Dereva wa Halmashauri kwa kosa la kudaganya elimu ya kidato cha Nne.
Pia taarifa hiyo ilieleza kuhusu Watumishi wanne Waliorejeshwa kazini ambao ni pamoja na John Shuka Mathias,ambaye ni Mtendaji wa Kijiji cha Mahando kwa kosa la utoro kazini, Maganya Shemu Kiyoya, Mtendaji wa Kijiji cha Lubili kwa kosa la utoro , na Godfrey H. Malogo ambaye ni Mtendaji wa Kata ambaye atapelekwa Mahakamani kwa kosa la upotevu wa mapato ya ndani ya shilingi Milioni 1,520,150/=, na George A. Sanga ambaye ni Dereva kwa kosa la kutotii mamlaka ambaye iliamuliwa apunguzwe mshahara kwa asilimia 15 kwa kila mwezi kwa miaka mitatu mfululizo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Misungwi Bi. Leokadia Humera amekiri kuwepo kwa maamuzi hayo ya Baraza la Madiwani ya kuwafukuza kazi Watumishi hao saba na kuwarejesha kazini Watumishi 4 kati ya 11 waliokuwa na mashitaka mbalimbali ya kiutumishi ambapo Tume iliundwa kuchunguza tuhuma zao kulingana na makosa waliyotenda na kuwasilisha taarifa katika mkutano wa Baraza la Madiwani uliopita.
Bi. Leokadia Humera amesema kwamba Halmashauri katika kipndi cha kuishia mwezi Julai 2021 imefanikiwa kukusanya fedha za mapato ya ndani yenye jumla ya shilingi Bilioni 2, 365, 911, 590.40 sawa na asilimia 102.87, na kutekeleza miradi ya maendeleo yenye jumla shilingi Bilioni 39, 310, 714,034.03 sawa na asilimia 89.12.ambapo miradi hiyo imekamilika na mingine inaendelea kukamilishwa.
Alifafanua mafanikio yaliyopatikana katika kipindi hicho ni pamoja na; ujenzi wa Kituo cha Afya cha Koromije ambacho kwa sasa kinatoa huduma za upasuaji pamoja na ujenzi majengo mawili katika Hospitali ya wilaya ya Misungwi. sambamba na ujenzi wa madarasa 26 vya madarasa, nyumba 3 za walimu pamoja na matundu 78 ya vyoo katika shule za msingi na kwa upande wa sekondari Halmashauri imefanikiwa kujenga vyumba 10 vya madarasa, maabara za Sayansi 3, na bweni 1 la wanafunzi wa kike katika Sekondari ya Misungwi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Mhe. Kashinje Machibya (wa pili kulia), akifatiwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bi.Leokadia Humera pamoja na viongozi wengine wa chama cha Mapinduzi (CCM) wakisikiliza na kufatilia mjadala katika mkutano wa Baraza la Madiwani Wilaya ya Misungwi.
Baadhi ya Madiwani wakiufatilia mjadala kwa umakini katika mkutano wa Barazala Madiwani katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.