Huduma za Usajili wa Leseni za Biashara
A. Mahitaji Muhimu wakati wa kupata Leseni mpya ya Biashara.
1. Fomu ya Maombi (Inapatikana Ofisi ya Biashara Wilaya)
2. Jina la/Majina ya Baishara (yataonekana kwenye leseni
yako).
3. Kama ni kampuni aje na nakala ya cheti ya usajili wa
BRELA (Certificate of Registration)
4. Nakala ya cheti cha namba ya utambulisho wa mlipa kodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA (TIN NUMBER).
5. Cheti Orijino cha kuonyesha hudaiwi kodi (Tax Clearance
Certificate) kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
6. Ada ya Maombi Tsh.1, 000/-
7. Ada za leseni kwa Mwaka (zinatofautina kulingana na aina ya
baishara)
Kwa usajili wa bishara zilizopo chini ya Mamlaka nyingine Mfano Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), biashara hizo ni kama vile Maduaka ya Dawa za Binadamu, Vinywaji laini, Maduka ya Pembejeo za Kilimo na Mifugo pamoja na maduka ya vyakula mnatakiwa kuwasilisha nyaraka zifuatavyo:-
(a). Cheti cha Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) au
Mamlaka nyingine
(b) Cheti cha Vipimo vya Afya
(c) Pamoja na viambatanishi vingine vilivyotajwa hapo juu.
B. Kwa wafanyabiashara ambao leseni zimeisha muda
wake/wanaohuisha (renew), wanatakiwa kuja na:-
1. Nakala ya leseni ya zamani (Iliyoisha muda wake)
2. Cheti halisi (Original) cha kuonyesha hudaiwi kodi toka Mamlaka ya
Mapato Tanzani-TRA (Tax Clearance Certificate)
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Afisa Biashara Wilaya ya Misungwi kwa simu namba:
0756824120
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.