Wednesday 15th, January 2025
@Uwanja wa Nyamagana Mwanza
Maadhimisho ya Mei MOSI mwaka 2017 yatafanyika katika ngazi ya Kimkoa katika Uwanja wa Michezo wa CCM Kirumba,Manispaa ya Ilemela, Jijini Mwanza na Mgeni Rasmi atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mhe, John Mongela,na kuhudhuriwa na watumishi wote,hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri kwa kushirikiana na Vyama vya Wafanyakazi wilaya ya Misungwi anawaalika wananchi wote kushiriki pamoja na Watumishi kusherekea siku ya Wafanyakazi Duniani.,
Ratiba rasmi ya Sherehe hizo itaanza saa 1.00 asubuhi kwa Maandamano ya Watumishi kutoka Uwanja wa Nyamagana kuelekea Uwanja wa Michezo wa CCM Kirumba na kupokelewa na Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.KAULI MBIU YA MEI MOSI mwaka 2017 ni "UCHUMI WA VIWANDA UZINGATIE KULINDA HAKI, MASLAHI NA HESHIMA YA WAFANYAKAZI".
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.