• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ardhi na Maliasili
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Maeneo ya Vivutio vya Utalii
    • Maeneo ya Kilimo
    • Maeneo ya Madini
    • Maeneo ya Uwekezaji wa Mazingira
  • Huduma Zetu
    • Huduma Sekta ya Afya
    • Huduma Sekta ya Elimu
    • Huduma Sekta ya Maji
    • Huduma Sekta ya Mazingira
    • Huduma Sekta ya Maendeleo ya Jamii
    • Huduma Sekta ya Ardhi na Maliasili
  • Baraza la Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Huduma za Kijamii
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba Vikao vya Halmashauri
  • Miradi mbalimbali
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Mbalimbali
    • Taratibu
    • Gazeti la Serikali
    • Taarifa
    • Fomu mbalimbali
    • Zabuni
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Video Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Habari Mpya

Hotuba

 Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2017-2018.pdf

 

 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

 

OFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

WILAYA YA MISUNGWI

 

 

 

 

 

 

TAARIFA FUPI YA WILAYA YA MISUNGWI KWA MHE, DR.JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

DESEMBA, 2016.

Imeandaliwa na:

Ofisi ya Mkuu wa Wilaya,

MISUNGWI

 

 

 

 

YALIYOMO

Jedwali Na.1: ENEO LA WILAYA KIUTAWALA NA SHUGHULI ZA WANANCHI. 5

DIRA YA HALMASHAURI. 6

DHIMA YA HALMASHAURI. 6

1.0 Hali ya Ulinzi na Usalama. 6

2.0   Hali ya Kisiasa. 6

3.0   Mapato Ya Ndani ya Vyanzo vya Halmashauri Kwa mwaka 2016/2017. 6

3.1UKUSANYAJI WA MAPATO YA NDANI KWA HALMASHAURI. 6

3.1.2 Mikakati ya ukusanyaji wa Mapato. 7

3.2 Ruzuku toka Serikali Kuu.. 8

SEKTA YA UCHUMI. 9

4.0        Uchumi wa Wilaya. 9

5.0 Sekta ya Kilimo. 9

5.1 Matumizi ya zana za kilimo. 9

5.2             Kilimo cha Umwagiliaji 9

5.3 Pembejeo za Kilimo: 10

5.3.1                  Pembejeo za Kilimo zenye Ruzuku ya Serikali: 10

Jedwali Na.5: Usambazaji wa Mbegu bora. 11

5.3 .2 Zao la Pamba: 11

5.4 Hali ya Kilimo na Chakula. 11

5.5 Mafanikio katika Sekta ya Kilimo: 13

5.6 Changamoto katika Sekta ya Kilimo: 13

5.7Mikakati ya kukabiliana na changamoto. 14

6.0    MIFUGO.. 14

7.0 SEKTA YA USHIRIKA: 15

8.0 Viwanda na Biashara. 17

8.1 Biashara. 17

8.2 Viwanda: 17

9.0        SEKTA YA UVUVI: 17

10.0 HIFADHI YA MAZINGIRA NA MISITU: 18

11.0   SEKTA YA MADINI NA NISHATI. 19

11.1 Sekta ya Madini 19

11.2 Hali ya Umeme Wilayani: 19

12.0 Ufugaji wa Nyuki 19

13.0  SEKTA YA ARDHI: 20

13.1     Masjala za Ardhi 20

13.2 Hali ya Uwekezaji na Uwezeshaji Wilayani: 20

13.3 Mikakati ya Halmashauri ya Wilaya kuhusu EPZ.. 21

13.4 Mafanikio. 21

14.0SEKTA YA MAENDELEO YA JAMII. 21

15.0 SEKTA YA MIUNDOMBINU.. 22

15.1   SEKTA YA MIUNDO MBINU.. 22

15.2 Hali ya barabara wilayani 22

15.3 Changamoto. 23

15.4 Jinsi ya kukabili changamoto. 23

15.5               VIVUKO: 23

HUDUMA ZA KIJAMII. 24

16 .0         SEKTA YA ELIMU: 24

16.1               Elimu ya Msingi 24

16.2 Idadi ya walimu katika Shule za Msingi hadi desemba 2016 2016: 26

16.2.1 Idadi ya walimu na upungufu: 26

17.0 ELIMU YA SEKONDARI. 27

17.1 CHANGAMOTO ZINAZOJITOKEZA KATIKA SEKTA YA ELIMU WILAYANI: 29

17.2 MIKAKATI YA UBORESHAJI WA ELIMU: 29

18.0 SEKTA YA AFYA: 30

18.1 AFYA YA MSINGI: 30

18.2  AFYA YA UZAZI NA MTOTO: 30

18.3UKIMWI: 30

18.4MALARIA: 31

18.5UPATIKANAJI WA DAWA NA VIFAA VYA TIBA KWENYE VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA: 31

18.6 CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI SEKTA YA AFYA WILAYANI: 32

18.7 Mikakati ya Kukabiliana na Changamoto: 32

19.0 USTAWI WA JAMII. 32

19.1  HUDUMA KWA WAZEE: 32

19.2 WATU WENYE ULEMAVU: 33

19.3   MAPAMBANO DHIDI YA MAUAJI YA ALBINO: 33

19.4   WATOTO WALIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI: 33

20.0 SEKTA YA MAJI. 34

21.1 MAJI MJINI. 34

21.1.1 TAARIFA YA HALI HALISI YA UTOAJI WA HUDUMA YA MAJI MJINI MISUNGWI. 34

21.2 Usambazaji wa maji Mjini (Mitindo Water Supply): 34

21.4 Changamoto: 35

21.5 Namna ya kutatua changamoto hizi (The wayforward). 35

22.0 MAJI VIJIJINI. 35

22.1 MIRADI YA MAENDELEO PROGRAMU YA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI (RWSSP)  36

22.2 Mchanganuo wa Miradi ya maendeleo;-. 36

22.3 Hali ya utekelezaji kufikia Septemba 30 2016 ni kama ifuatavyo:-. 36

22.4 Ujenzi wa Mradi wa Maji bomba wa Ngaya hadi Matale. 37

22.5 Hali ya utekelezaji kwa sasa ni kama ifuatavyo. 37

22.6          Ujenzi wa Mradi wa Maji bomba wa Matale –Manawa-Misasi. 37

22.7 Hali ya utekelezaji kwa sasa ni kama ifuatavyo:-. 37

22.8 Changamoto za Idara katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo. 38

22.9 Utatuzi wa Changamoto. 38

23. 0 HALI YA UTUMISHI KATIKA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA.. 39

23.1     HALI YA UTUMISHI: 39

23.2 UPANDISHWAJI VYEO: 39

23.3 CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI SEKTA YA UTUMISHI: 39

23.4 TAARIFA YA UHAKIKI WA WATUMISHI. 40

24.0 Huduma za Fedha Zinazotolewa na Taasisi mbalimbali 40

25.0 Mawasiliano. 40

26.0 Hitimisho. 40

 

 

TAARIFA FUPI YA WILAYA YA MISUNGWI KWA MHE, DR.JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI, RAIS YA JAMHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA.

DESEMBA, 2016.

UTANGULIZI                               

Jedwali Na.1: ENEO LA WILAYA KIUTAWALA NA SHUGHULI ZA WANANCHI

Mwaka wa kuanzishwa Wilaya

1995

Eneo:
Eneo la Wilaya kwa ujumla (Km2)

2,553

Eneo kavu (Km za mraba)

2,378

Eneo la Maji (Km za mraba)

175

Mahali Wilaya ilipo:
Latitude Kusini mwa Ikweta

2º 35’ na 3 º15’

Longitude Mashariki mwa Greenwich

33º 15'

Hali ya hewa:
Hali ya joto liko kati ya nyuzi

25°C na 30°C

Hali ya mvua (mm)

500 – 700

Mvua za vuli na masika hunyesha kati ya miezi ya

Okt – Des, Machi – Mei

Idadi ya watu:
Watu wote

351,607

Wanaume

173,997

Wanawake

177,610

Ongezeko la watu kwa mwaka

2.8%

Idadi ya Kaya

54,093

Idadi ya watu kwa kila kaya

6.5

Mgawanyo wa kiutawala:

Idadi ya Majimbo ya uchaguzi

1

Tarafa

4

Kata

27

Vijiji

113

Vitongoji

724

Idadi ya shule za msingi
Shule binafsi                                       7
Shule za serikali                              138
Idadi ya shule za sekondari
Shule binafsi                                        4
Shule za serikali                                23
Idadi ya vituo vya afya
                                                            4
Idadi ya zahanati
Zahanati  za binafsi                             2
Zahanati  za serikali                          38
Idadi ya Hospitali
Hospitali ya  binafsi                             1

Hospitali ya Serikali                             1        

DIRA YA HALMASHAURI

“Dira ya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ni kuwa na Maisha bora kwa watu wake kwa kuwapatia huduma endelevu za kijamii na kiuchumi kwa misingi ya utawala bora.”

DHIMA YA HALMASHAURI

“Dhima ya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ni kuhakikisha kuwa jamii na wadau wote wanashiriki kikamilifu katika kupata huduma endelevu za kiuchumi na kijamii kwa kutumia rasilimali na mazingira yaliyopo yakiwemo ya utawala bora.”

1.0 Hali ya Ulinzi na Usalama

Hali ya ulinzi na usalama ni shwari licha ya kuwepo kwa matukio ya uvunjifu wa amani yanayojitokeza mara kwa mara.

2.0   Hali ya Kisiasa

Hali ya kisiasa wilayani kwa ujumla ni shwari, uhusiano kati ya vyama vya siasa vilivyopo na Serikali ni mzuri. Hali hii imewezesha shughuli za maendeleo kutekelezwa vizuri.

3.0   Mapato Ya Ndani ya Vyanzo vya Halmashauri Kwa mwaka 2016/2017

3.1UKUSANYAJI WA MAPATO YA NDANI KWA HALMASHAURI

Katika Mwaka wa fedha 2016/2017 Halmashauri ilikadiria kukusanya kiasi cha shilingi 1,601,368,000.00 kutoka katika vyanzo vyake vya mapato ya ndani.Hadi kufikia tarehe 30 Novemba, 2016,Halmashauri imeshakusanya jumla ya shilingi 499,413,128.42 ambayo sawa na asilimia 31.19 .Hata hivyo Halmashauri ipo nyuma kwa asilimia 9.8 katika makusanyo kutokana na  kutoletewa  kwa gawio asilimia 30 kutoka wizara ya ardhi ambacho ni chanzo kimojawapo, kodi ya majengo bado haijaanza kukusanywa  kutokana na kwamba Halmashauri bado ipo katika maandalizi ya kisheria.Vyanzo vikuu vya mapato ya ndani kwa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi ni ushuru wa kokoto na mchanga, ushuru wa stendi ,ushuru wa magulio , minada ya mifugo, kodi ya ardhi,kodi ya majengo na ushuru wa huduma.

3.1.2 Mikakati ya ukusanyaji wa Mapato

Kuiomba serikali iangalie upya swala la ulipaji wa ushuru wa huduma (service levy) kwani makampuni yanayofanya kazi hapa hususani makampuni ya uchimbaji kokoto na mengine yamekuwa yakilipia ushuru katika makao makuu ya ofisi zao yaliyopo jijini Mwanza na wakati shughuli hizo zinafanyika katika wilaya ya Misungwi.

Kuna sheria ambazo zimepitwa na wakati. Aidha kuanza mchakato wa utungaji wa sheria ndogo ili kuongeza mapato.

Kuomba serikali iongeze safari za magari madogomadogo ya abiria toka Mwanza mjini hadi Nyashishi ambapo tuna eneo la stendi, lakini halifanyi kazi kutokana na kukosekana kwa route hiyo.

Uboreshaji wa Takwimu za vyanzo mbalimbali vya mapato.

Kuboresha Ushikiano wa Wadau, Maafisa Watendaji wa Kata na Waheshimiwa Madiwani katika ukusanyaji wa mapato.

Kubaini vyanzo vipya vya mapato ambavyo bado havijafikiwa kutoka ngazi ya Kata, Vijiji na Vitongoji hii ni pamoja na kuandaa rejista za ukusanyaji wa mapato kwa kila chanzo kilichopo kwenye kata.

Jeshi la polisi kushirikishwa ipasavyo  ili kusaidia ukusanyaji wa mapato katika vyanzo mbalimbali vya Halamshauri

Kufanya kazi kwa ushirikiano na wadau, watendaji, na waheshimiwa Madiwani ili kuwa na ukusanyaji wenye tija (Team work), Aidha wadau kama TRA , Madini na TMAA  kutoa takwimu  zitakazosaidia ukadiriaji  wa vyanzo mbalimbali vya mapato

Watumishi na wakala wanaohusika katika ukusanyaji wa mapato kujengewa dhana ya uaminifu kwa wakusanyaji wa mapato.

Uboreshaji na uanazishaji wa huduma za msingi kwa wananchi ikiwemo magulio ya Halamshauri na vyanzo vingine ili kuchangia hali ya wananchi kuotoa tozo mbalimbali za Halamshauri

Ubunifu katika kukusanya mapato, ambao utaruhusu wadau mbalimbali kufanya uboreshaji katika maeneo mbalimbali.

Kuwatumia watendaji wa kata na vijiji vizuri kudhibiti mianya ya utoroshaji wa mazao hasa wale wanaoficha mazao katika miji ya watu. Yule atakayekamatwa anaficha mazao alipie asilimia fulani kama adhabu.

Wafanyabiashara waandikishwe na kuorodheshwa ili kila mmoja awajibike kulipa kodi. Kazi hii ifanywe na watendaji wa kata na vijiji

Ujenzi wa choo katika gulio la Mabuki

Mashine za EFD /POS kutotumika kwa ukamilifu, hivyo elimu izidi kutolewa juu ya suala zima la uaminifu.

Kutoa kipaumbele katika ulipaji wa Kodi ya majengo na ardhi ili iweze kulipwa ipasavyo

Kuboresha sheria ndogo zilizopitwa na wakati hasa za ukusanyaji wa mapato ili tuweze kuboresha Halmashauri yetu .

3.2 Ruzuku toka Serikali Kuu

Katika kutekeleza mpango wa maendeleo wa Halmashauri ya Wilaya kwa mwaka wa fedha 2016/2017, Halmashauri ya wilaya imepanga kutumia kiasi cha Tshs.

10, 861,714,709.18 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika  sekta za Afya, Elimu, Maji, Ardhi, Ujenzi, Mipango, Kilimo/Mifugo na Utawala.Fedha hizo zitatoka katika vyanzo mbalimbali navyo ni Serikali Kuu, Halmashauri ya Wilaya, Busket Fund, NRWSSP, Mfuko wa Jimbo, SEDP, TASAF, TACAIDS, Road Fund, LGCDG na michango ya jamii.

Hadi kufikia tarehe 30 Novemba 2016, Halmashauri ya wilaya imepokea  jumla ya kiasi cha Tshs 2,385,720,866  za miradi ya maendeleo ambayo ni sawa na asilimia 23.50 .Fedha hizi zimetolewa na vyanzo mbalimbali ambavyo ni serilkali kuu,LGCDG, na TASAF kwa mchanganuo ufuatao: kiasi cha  Tshs 300,000,000 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule za msingi  ambazo ni Mitindo,Busagara na Misungwi (Shule maalumu) kutoka Serikali kuu,imepokea  Tshs. 368,700,000 kwa ajili ya kuboresha elimu ya msingi  pia toka serikali kuu.Sambamba na hilo halmashauri imepokea Tshs 221,565,000 toka LGCDG,imepokea Tshs 23,917,000.00 za mfuko wa jimbo, imepokea tshs  1,255,351,500 .00 toka TASAF,imepokea Tsh 216,187,183.16 za miradi wa sekta ya maji vijijini. Hata hivyo kiasi cha Tshs.1,034,834,500.00 kimetumika ambayo ni sawa na asilimia 43.37% ya fedha zilizopokelewa hadi sasa.

 

SEKTA YA UCHUMI

4.0       Uchumi wa Wilaya

Pato la wananchi kiwilaya limekuwa likiongezeka kwa asilimia tano na kinachochangia kuongezeka huko ni uwepo wa shughuli za kilimo, wachimbaji wadogowadogo wa madini, uvuvi, ufugaji, shughuli za biashara na taasisi za umma. Kwa mwaka 2012 pato la mwananchi mmoja mmoja wa Wilaya ya Misungwi linakadiriwa kufikia 647,777.00 kwa mwaka na hivyo kufanya Pato la wilaya kuwa shilingi 455,103,461.00 (Sensa ya mwaka 2012.)

5.0 Sekta ya Kilimo

5.1 Matumizi ya zana za kilimo

 

Jedwali Na.2: Matumizi ya Zana za Kilimo

 

 

Wilaya/Halmashauri

 

 

Idadi ya matrekta

Asilimia ya wakulima wadogo wanaolimia matrekta

 

Idadi ya plau

Asilimia ya wakulima  wanaotumia plau

Idadi ya wakulima wanaotumia jembe la mkono

 

 

%

 

 

P.Tiller

 

 

%

Misungwi
119
8
5,730
43
202788
47
48
2
Jumla  
119
8
5,730
43
135,825
47
48
2

 

5.2       Kilimo cha Umwagiliaji

 

Halmashauri ya Wilaya ina eneo linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji lenye ukubwa wa Ha 8,969.Aidha Halmashauri ya Wilaya inazo skimu 6 za kilimo cha umwagiliaji zenye ukubwa wa Ha.  2,975.Ambapo  Skimu 3  zinalimwa na kumwagilia nazo ni Igongwa yenye Ha 240 zinazomwagilia,Ilujamate yenye Ha 75 zinazomwagilia ,Nyashidala Ha 220 zinazomwagilia na skimu 3  hazifanyi kazi  nazo ni Nyambeho yenye Ha 200 ambayo miundombinu yake iliondolewa na mafuriko y mwaka 2006, Igenge yenye Ha 200 Mradi haujakamilika  na umesimama muda mrefu na Mbarika yenye Ha 200 ulisimama.  

 

 

 

 

 

  •  
  •  
  •  
  • Jedwali Na.3:  Ukubwa wa maeneo ya umwagiliaji kwa Hekta,Wilaya ya Misungwi 2016
  •  
  • Wilaya
  • Eneo linalofaa umwagiliaji(Ha)
  • Eneo linalotumika  kwa umwagiliaji (Ha)
  • Asilimia ya matumizi ya umwagiliaji
  • Misungwi
  • 8,969
  • 535
  • 5.9
  • Jumla
  • 8,969
  • 535
  • 5.9

 

 

5.2.1 Changamoto umwagiliaji

  • Ujenzi wa Miradi ya umwagiliaji kutokamilika ambapo imepelekea upotevu wa maji na wananchi kutofaidika na miradi hiyo hivyo kubaki katika hali ya umasikini mfano mradi wa Igenge,Igongwa,Nyambeho,Ilujamate na Nyashidala na Mbarika  haijakamilika hadi sasa.
  • Miradi ya umwagiliaji haina vyanzo vya kudumu vya uvunaji wa maji, hivyo kutegemea uwepo wa mvua.
  • Wakulima kutolinda miundombinu ya umwagiliaji iliyopo.mfano mradi wa umwagiliaji wa Nyashidala, ambapo wananchi wanafanya uharibifu wa miundombinu hiyo.

 

  • 5.2.2 Mikakati katika umwagiliaji
  • Zoezi la uibuaji wa miradi kwa kushirikiana na wafadhili wa kutoka JAPAN katika mradi wa TANCAID 2 linaendelea.Ambapo awali wananchi hawakushiriki kikamilifu  katika uibuaji wa miradi ya umwagiliaji,lakini kwa sasa wameshirikishwa kikamilifu.
  • Halmashauri inaendelea kutenga fedha wa kuendeleza mradi wa Igenge ili uweze kukamilika.
  • Kuhamasisha wananchi ili watambue miradi kuwa ni mali yao .

 

5.3 Pembejeo za Kilimo:

5.3.1    Pembejeo za Kilimo zenye Ruzuku ya Serikali:

 Wilaya ya Misungwi haikupata mgao wowote wa Pembejeo zenye Ruzuku ya Serikali (Mbolea na Mbegu), isipokuwa wakulima wananunua kwenye maduka ya pembejeo ya wafanya biashara binafsi.

 

Jedwali Na.4: Mbolea iliyonunuliwa na wakulima mwaka 2013/14 hadi 2016/17 (TANI)

Namba

Aina

2013/2014

2014/2015

2015/2016

2016/2017

1
UREA

57

65

73

98

2
CAN

60

64

76

82

3
S/A

0

0

0

0

4
NPK

23

28

33

41

5
MINJINGU

0

0

0

0

JUMLA

140

157

182

221

Jedwali Na.5: Usambazaji wa Mbegu bora

Namba
Aina

2013/2014

2014/15

2015/2016

2016/2017

1
Pamba

88.012

192

195

315.05

2
Mahindi

31

39

45

57

3
Mpunga

0

0

0

0

4
Mtama

0.570

0.530

0.410

0.113

5
Alizeti

0

0

0

6

6
Bustani

1.5

2

2.5

3.2

JUMLA

121.082

233.530

242.910

381.363

 

5.3 .2 Zao la Pamba:

Wilaya imehamasisha wakulima kujiunga na kilimo cha mkataba cha pamba ili waweze kukopeshwa pembejeo. Jumla ya tani 315.05 za mbegu ya pamba zimesambazwa vijijini ambapo jumla ya tani 168.12 zimekopeshwa kwa wakulima. Hata hivyo kutokana na upungufu wa mvua, wakulima wengi hawajapanda mbegu hizo.

5.3.3 Zao la Alizeti

Ili kuhamasisha kilimo cha alizeti, wilaya imenunua jumla ya tani 6 za mbegu ya alizeti, mbegu hizo zimesambazwa kwa wakulima. Baada ya mavuno kila mkulima atarudisha kiasi cha mbegu alichopewa ili na wakulima wengine waweze kupewa mbegu hizo.

5.4 Hali ya Kilimo na Chakula

Wilaya ya Misungwi imekuwa ikijishughulisha na kilimo katika maeneo mbalimbali ingawa hali ya hewa na mwenendo wa mvua si wa kuridhisha. Hali halisi ya utekelezaji katika sekta hii ikihusisha eneo la kilimo, matumizi ya zana za kilimo na ununuzi wa matrekta.

5.5.1 Upatikanaji wa chakula 

Chakula  aina ya Nafaka  ( Mahindi, Mpunga, na  mtama na mawele ), vyakula vya  mizizi ( Mihogo na viazi vitamu vibichi ) pamoja na vyakula aina ya  mikunde vinapatikana katika masoko na magulio yaliyomo wilayani.  Vyanzo vya upatikanaji wa mazao hayo ya chakula ni kutoka ndani ya wilaya na kiasi kidogo kutoka nje ya wilaya hasa kwa zao la mikunde aina ya maharage ndizi za kupika na mbivu, viazi mviringo, unga wa ngano  na Matunda aina ya nanasi.

Jedwali Na.6: MAHITAJI YA CHAKULA KWA MWAKA 2016 / 2017.

Idadi ya watu
Aina ya chakula
Mahitaji  kwa mwaka
Uzalishaji
2015 / 2016
Upungufu /  Ziada
 ( Tani )
Maelezo
(Sensa ya 2012)  326,503
Nafaka ( wanga )
89,380
100,989.30
+ 11,609.3
Januari 2017 kutakuwa na upungufu wa chakula kwa sababu mazao yaliyopandwa mwezi Octoba hayakupata mvua za kutosha, hivyo mavuno ya mazao hayo yatakuwa kidogo na kusababisha upungufu wa chakula.
Mikunde ( Protini )
8,938
9,250.1
+ 312.1

 

5.5.2 Mikakati ya kukabiliana na hali ya chakula

  • Wananchi wameelimishwa kutunza chakula walicho nacho kwa sasa
  • Wananchi wamehamasishwa kupanda mazao yanyovumilia ukame endapo tutapata mvua mwezi Januari, 2017
  • Kuuza mifugo waliyonayo ili waweze kununua chakula
  • Wananchi wameelimishwa wasiuze chakula kwa wafanya biashara wanaopeleka chakula nje ya nchi.

5.5.3 BEI YA VYAKULA KUISHIA NOVEMBA, 2016

Bei ya vyakula mbalimbali (vyakula aina ya nafaka, mizizi na mikunde  vinapatikana na kuuzwa katika masoko na magulio wilayani kwa bei ya kutofautiana  kati ya soko na soko/ gulio na gulio.

Jedwali Na 7: Jedwali lifuatalo hapo chini linaonyesha wastani wa bei ya vyakula kuishia Novemba, 2016 

 

Aina ya chakula

Upatikanaji wake

MAELEZO / AINA YA KIPIMO

Ndani ya Wilaya

Nje ya Wilaya

Novemba
     2016

Mahindi   ⃰  

√

√

12,000/-

Kwa Ndoo ya  kilo 20
Mtama

√

0

9,900/-

Kwa Ndoo
Uwele

√

0

9,900/-

Kwa Ndoo
Mpunga

√

0

9,900/-

Kwa Ndoo
Mchele    ⃰

√

0

1,200/-

Kwa Kg.
Muhogo( udaga)

√

0

8,000/-

Kwa Ndoo
Viazi vitamu- vibichi

√

0

500/-

Kwa kg
Viazi vitamu- vikavu

√

0

700/-

Kwa kg
Choroko

√

0

2000/-

Kwa kg
Maharage   ⃰

√

√

2,000/-

Kwa Kg
Dengu

√

0

2000/-

Kwa kilo
Karanga(menywa)

√

√

2,500/-

Kwa kilo
Karanga ( maganda)

√

0

9,000/-

Kwa Ndoo
Njugumawe

√

√

3,000/-

Kwa kg.
Kunde

√

0

1,600/-

Kwa kg
Viazi Mviringo

0

√

1,000/-

Kwa kg
Ndizi za Kupika

0

√

1,200/-

Kwa kg

 * Chakula kikuu   

             

5.4 MALENGO YA KILIMO MSIMU 2016/17

            

Jedwali Na.8: Kilimo cha Mazao ya chakula na Biashara : Wilaya msimu huu imeweka Malengo ya kilimo katika msimu huu 2016/17. Malengo hayo ni kama ifuatavyo:-

Aina ya              Zao

Lengo
Utekelezaji wa malengo na matarajio ya mavuno hadi sasa

Maelezo

Eneo(Ha)
Mavuno (Tani)
Eneo(Ha)

% ya utekelezaji

Mavuno (Tani)

Mtama
10,550.9
10,129

698



 
Utekelezaji wa malengo haya utaanza mwezi wa Novemba 2016.
 
 
Mvua zimechelewa kuanza.
 
 
 
 
Uwele
5,199.3
5,199.3

243



Mpunga
26388.3
53,304

1,373.75



Mahindi
33,258.2
42,238

11,796



Muhogo
23,067.2
35985

2,366.5



Viazi vitamu
22,017.5
35,228

1529



Choroko
14,900.2
8,195

2,523.7



Kunde
6531.7
2743

384



Maharage
6568.55
3,219

472.5



Njugu mawe
4690.05
2486

150.2



Jumla- mazao ya chakula
153,171.90
198,726

21,536.65

 

 
Pamba
6,739
4,515.1

4175.7



Karanga
9355.2
5,332

818.2



Dengu
20,383.4
16,103

103



Alizeti
3039
1914.6

94



Jumla mazao ya biashara
39,517
27,864.70

5190.9

 

 

 

5.5 Mafanikio katika Sekta ya Kilimo:

Asilimia 70 ya wakulima wote wamehamasika kutumia pembejeo (madawa na mbolea) pamoja na   kulima kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo.

Wakulima wamehamasika kununua zana za kilimo kama vile Trekta kubwa na ndogo kwa kupitia  njia ya mikopo.

Wakulima, vikundi na taasisi wamehamasika kulima mazao ya pamba na alizeti.

5.6 Changamoto katika Sekta ya Kilimo:

Mvua zinazonyesha msimu huu wa vuli siyo za kuridhisha  hivyo kutakuwepo na upungufu wa mavuno.

Bei za mazao ya mazao ya chakula hasa mahindi imepanda toka Tsh. 12,000 mwezi Novemba 2016 hadi Tsh. 16,000 mwezi Desemba kwa debe la kilo 20.

5.7Mikakati ya kukabiliana na changamoto

Kuwaelimisha wakulima kuzingatia kanuni bora za kilimo ili waweze kuongeza tija katika uzalishaji.

Kuhakikisha kila kaya inajitosheleza kwa chakula  na kupata ziada  kwa  ajili ya kuuza, pia  kuwahimiza wakulima  kulima mazao yanayostahimili ukame angalau kila kaya kulima ekari moja ya mtama/uwele au mihogo.

Kuhamasisha jamii kupanda  miti ambayo ni rafiki kwa  mazingira, hii itasaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Kuunganisha wakulima  na tasisi mbalimbali  zinazokopesha zana za kilimo hususani matrekta.

Kuwawezesha wakulima kupima mashamba yao ili kupata hati miliki za kimila ambazo zitawawezesha kukopa.

6.0    MIFUGO

 Wilaya ina jumla ya eneo la Ha. 96,000 ambalo linafaa kwa malisho ya mifugo. Idadi ya mifugo iliyopo ni 175,708 idadi hii inajumuisha Ng’ombe, Mbuzi na Kondoo. Hata hivyo maeneo mengi hayafai kwa ufugaji kutokana na kuwepo na ukosefu wa maji hasa wakati wa kiangazi. Wilaya inaendelea kutoa elimu ya kutumia madume bora na uhamilishaji ili kupata mifugo michache yenye tija kwa lengo la kujaribu kuwatoa katika kundi la uchungaji kuwa wafugaji, vilevile elimu ya upandaji na hifadhi ya malisho hutolewa mara kwa mara. Aidha wananchi wamekuwa wakihimizwa kuogesha mifugo yao ili kuepukana na magonjwa ya mifugo na chanjo hutolewa kudhibiti magonjwa ya milipuko na kuambukiza

Jedwali Na 9:  IDADI YA MIFUGO WILAYANI

Wilaya

Idadi ya mifugo

 

 

 

 

Eneo linalotumika kwa malisho (Ha)

Uwezo wa malisho

(carrying capacity)

Ng’ombe
Mbuzi
Kondoo

Mbwa

Nguruwe

Punda

Kuku

Misungwi
131,250
34,214
10,224
10,336
942
801
194,556
96,000
1.966
Jumla 
131,250
34,214
10,244
10,336
942
801
194,556
96,000
1.966

 

7.0 SEKTA YA USHIRIKA:

Ili kupambana na umaskini wananchi wanaelimishwa na kuhimizwa kujiunga katika vikundi ili kukusanya nguvu na kutatua matatizo yanayowakabili katika uzalishaji na masoko. Katika jitihada hizo Wilaya ya Misungwi imekuwa na jumla ya vyama vya ushirika 144 vya aina mbalimbali. Aina ya vyama vilivyopo ni SACCOs (Savings and Credit Co operatve Society)  89, AMCOs (Agricultural Marketing Co operative Socities) 40, ushirika aina nyingine viko 15 VICOBA (Village Community Banks) viko 30, pia kuna aina nyingine ya vyama.

Vilevile Wilaya imeweka mkazo zaidi katika vyama vya Akiba na Mikopo na ambapo jumla ya mikopo yenye thamani ya shilingi 2.4 bilioni tayari imeshakopeshwa kwa wanachama wake.

 

Jedwali Na.10:  IDADI YA VYAMA VYA USHIRIKA KATIKA WILAYA HADI NOVEMBA 30, 2016

Aina ya Chama

Misungwi

Jumla

Vyama vya mazao (AMCOS)

40

40

SACCOS

89

89

Usafirishaji

1

1

Huduma

-

-

Maduka

0

0

Viwanda

4

4

Ushirika Shughuli Nyingi

0

0

Uvuvi/samaki

4

4

Nyumba

0

0

Ujenzi

1

1

Madini

1

1

Umwagiliaji

4

4

Vyama vinginevyo

0

0

Vyama vikuu

0

0

Jumla

144

144

 


Jedwali Na.11: HALI YA VYAMA VYA USHIRIKA VYA AKIBA NA MKOPO (SACCOS) KUISHIA TAREHE 30 NOVEMBA, 2016

HALMASHAURI

IDADI YA

MTAJI

MIKOPO

SACCOS

WANACHAMA

HISA

AKIBA

AMANA

JUMLA

TOLEWA

REJESHWA

BAKI

Misungwi
89
91,125
288,100,010
194,800,347
85,000,800
567,901,157
2,400,906,600
960,540,000
1,440,360,600
Jumla
89
91,125
288,100,010
194,800,347
85,000,800
567,901,157
2,400,906,600
960,540,000
1,440,360,600

 


8.0 Viwanda na Biashara

8.1 Biashara

Halmashauri ya Wilaya inashirikiana na TCCIA ili kuimarisha biashara katika sekta binafsi.

Aidha wakulima na wafanya biashara wilayani wanashiriki katika mashindano ya nane nane pamoja na soko la Afrika Mashariki yanayofanyika kimkoa na Kitaifa na kimataifa kila mwaka kuonyesha bidhaa zao ili kupanua soko.

Elimu ya utaratibu wa uanzishaji wa Biashara inatolewa kwa wafanyabiashara kila mwaka ili kufanikisha urasimishaji wa Biashara kwa utoaji wa Leseni za Biashara. Elimu hii hutolewa kwa Umma kwa kutumia vipeperushi na matangazo kwa kutumia vipaza sauti.

8.2 Viwanda:

Wilaya imetenga eneo la uwekezaji lenye ukubwa wa Hekta 2400 katika vijiji vya Nyang’homango na Mwasonge Tarafa ya Usagara, pia Halmashauri ya Wilaya imetenga ekari 83 eneo la Somanda Misungwi mjini kwa ajili ya maendeleo ya viwanda.

Jumla ya vikundi vitatu (3) vya usindikaji vimepatiwa mafunzo navyo ni Nyota Group cha maziwa na ngozi, Inonelwa cha kusindika ngozi na Alovera Upendo cha Mabuki kinachosindika mvinyo. Aidha wajasiriamali wanaozalisha viazi Carrot wameunganishwa na makampuni makubwa yanayotengeneza biscuits.

9.0       SEKTA YA UVUVI:

Wilaya ya Misungwi ina eneo lenye kilomita za mraba 175 ambapo lipo ndani ya ziwa victoria. Eneo hilo la ziwa lina jumla ya wavuvi 1,369 na mitumbwi 345 kwa takwimu za mwaka 2014 . Wadau wa uvuvi 281walipata elimu juu ya uvuvi wa kisasa katika vijiji vya kandokando ya ziwa. Vikundi 10 vya uvuvi shirikishi yaani (Beach Management Units) BMU vinaendelea kuimarishwa.

Katika kipindi cha miaka mitano (2012- 2016)  jumla ya mabwawa ya kufugia samaki 101 yamechimbwa katika vijiji vya Mwaniko (4), Mbarika  (14), Kigongo (13), Ilalambogo (6), Lugobe (6), Mwalogwabagole (26), Mwajombo (12), Nyang’homango (6), Misungwi (4), Sawenge (4),Magaka (2) na Nyamatala (4).

Uvunaji wa samaki umekuwa ukipungua kuanzia mwaka 2012 hadi mwaka 2016 hii ni kutokana na jitihada zinazofanywa na wilaya za kuhakikisha kuwa uvuvi haramu unakomeshwa,  kabla ya jitihada za kukomesha uvuvi haramu takwimu zilikuwa juu sana kwakuwa hata wale samaki ambao hawakutakiwa kuvunwa walikuwa wanahesabiwa, mabadiliko ya hali ya hewa, kupungua kwa kina cha maji ziwani, kilimo cha kandokando ya ziwa na matumizi mabaya ya dawa za kilimo na mifugo. Aidha eneo la Ziwa Victoria lililopo upande wa Misungwi ni maalum kwa ajili ya uzalishaji samaki (Breading site) hivyo shughuli za uvuvi zinasimama kipindi cha mwezi Januari hadi Juni yaani ziwa hufungwa.

10.0     HIFADHI YA MAZINGIRA NA MISITU:

Maeneo yanayostahili kuhifadhiwa yapo, mfano misitu ya hifadhi ambayo ipo chini ya Halmashauri (Local authority forestry reserves) ambazo ni Mamani km za mraba 758, sisu km za mraba 921, malenge km za mraba 220 na Ilangafipa km za mraba 1,336. Hata hivyo ukubwa wa eneo uliooneshwa ni wa hapo awali na umepungua kutokana na uchomaji ovyo, ukataji wa miti, upanuzi wa makazi, ufugaji na kilimo na Uchimbaji wa Dhahabu.

Vijiji vilivyopo katika mpango wa usimamizi shirikishi wa mazingira ni vile vilivyo na hifadhi za uoto wa asili, taasisi na shule. Wastani wa upandaji miti kwa kwa mwaka ni miti 1,008,900 na miti inayostawi ni wastani wa miti 898,213

 

  • Jedwali Na.12: Upandaji Miti Kwa Kila Mwaka Katika wilaya ya Misungwi.

Wilaya

2013/2014

2014/2015

2015/2016

2016/17

Misungwi
634,700
897410
1,276,189
1,300,00,000
JUMLA
634,700
897410
1,276,189
 

 

11.0   SEKTA YA MADINI NA NISHATI

11.1 Sekta ya Madini

Wilaya ya Misungwi ina maeneo yenye madini ya Dhahabu ambapo wachimbaji wadogo zaidi ya 400 wamekuwa wakijihusisha na uchimbaji wa madini hayo katika maeneo ya Ishokera na Mwamazengo. Pia Wilaya ina madini ya Almasi katika kijiji cha Mwanangwa.Aidha Wilaya ina makampuni yanayoponda kokoto na maeneo ya mchanga katika kijiji cha Nyang’homango, Isamilo, Mwasonge, Fella, Ntende na Usagara

Hata hivyo Halmashauri inaendelea kuhamasisha wachimbaji wadogo wadogo kuunda na kusajiri vikundi vya uchimbaji ili waweze kupata mikopo katika taasisi za kifedha

11.2     Hali ya Umeme Wilayani:

 

Wilaya imeunganishwa na umeme wa Grid ya Taifa (Tanesco). Umeme huu unapatikana katika miji ya Misungwi, Usagara, Bukumbi, Misasi na Koromije. Hata hivyo vijiji mbalimbali vimepata umeme kupitia mradi wa umeme vijijini (Rural Electrification Agency – REA)  na Electricity 5.

12.0 Ufugaji wa Nyuki

  • Hamasa imetolewa katika tarafa zote za Wilaya ya Misungwi na walioonesha mwitikio wa haraka ni Kata za Lubili, Ukiriguru, Bulemeji, Misungwi, Koromije na Igokelo.
  • Vikundi 18 vimeonyesha nia ya kufuga nyuki toka katika vijiji 9 vya Nyamayinza, Buganda, Ukiriguru, Mapilinga, Ng’wakitolyo, Ibongoya ‘A’, Bugomba na Misungwi.
  • Mizinga 1715 kutoka Tara yote imekwisha chongwa ikiwa 998 ni kwa watu binafsi, Taasisi 17 na 700 vikundi.
  • Mabanda 5 yalijengwa ikiwa mawili (2) yapo Misungwi Makao Makuu, moja (1) ni Ngudama (TASAF), moja (1) kikundi cha Nyota cha Misungwi na moja (1) ni kikundi cha Bujingwa. Kwa sasa kuna mabanda mawili (2) mengine yameharibika.

Kwa sasa Halmashauri inatarajia kuhakikisha kuwa inatenga bajeti ili kuendelea na utekelezaji wa azma hiyo. Jedwali lifuatalo linaonesha mchanganuo wa mizinga nyuki Wilayani.

Jedwali Na.13: Mchanganuo wa Mizinga ya nyuki Wilayani

Aina ya Mizinga ya Nyuki

Idadi

Wamiliki

Mizunga ya asili
400
Watu binafsi
Mizinga ya kisasa kabla ya maelekezo ya Dododma
130
Watu binafsi na kikundi kimoja
Mizinga ya kisasa baada ya maelekezo ya Dodoma kufikia leo
1715
  • Watu binafsi – 998
  • Watu binafsi na viikundi – 700
  • Taasisi - 17
Jumla kuu
2245

13.0     SEKTA YA ARDHI:

13.1     Masjala za Ardhi

Halmashauri ya wilaya ina masjala za ardhi  3 zilizokamilika na zinatoa huduma katika vijiji vya Kasololo, Isamilo na Matale. Masjala za Kasololo na Matale zilipata fedha kwa ajili ya kuandaa matumizi bora ya ardhi kupitia mradi wa MKURABITA na Idadi ya mashamba yaliyopimwa kupitia MKURABITA  ni 1,341 kwa vijiji vyote viwili, katika kijiji cha Kasololo mashamba 863 yalipimwa na Matale mashamba 478 yalipimwa na mashamba 548 yameshaingizwa katika kompyuta kwa hatua ya uandaaji wa Hati. Mpaka sasa idadi ya Hati zilizoandaliwa ni 793 ikiwa Hati 474 ni za kijiji cha Kasololo na Hati 319 ni za kijiji cha Matale.

Aidha Wilaya inaendelea kuhamasisha wananchi kuweza kupimiwa maeneo yao ili kuweza kupata Hati miliki zitakazo wawezesha kupata utambulisho na udhamini katika masuala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.

13.2 Hali ya Uwekezaji na Uwezeshaji Wilayani:

Halmashauri ya wilaya ya Misungwi imeunda kitengo cha uwekezaji chenye waatalamu 3.Ambapo walishajengewa uwezo na wataalamu wa EPZA. Halmashauri imeshatenga eneo la uwekezaji katika kata za Ukiruguru na Bulemeji. Ukubwa wa eneo lililotengwa kwa matumizi ya mradi huu wa EPZ ni takribani hekta 2,400.Hata hivyo  uhamasishaji umefanyika kwenye maeneo haya,  Watendaji wa Halmashauri na wajumbe wa kamati ya fedha wamejengewa uwezo  juu uwekezaji wa viwanda na wataalmu kutoka EPZA.

13.3 Mikakati ya Halmashauri ya Wilaya kuhusu EPZ

Mikakati ya Halmashauri ya Wilaya kuhusu eneo la EPZ ni kama ifuatayo:-

Kwa kuwa maeneo haya yameendelea kuendelezwa na wananchi, Halmashauri inaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kulipia fidia kwa awamu.

13.4 Mafanikio

  • Halmashauri ya Wilaya imeweza kutenga eneo hekta 2400 lililopo katika kata 2 Bulemeji na Ukiruguru.
  • Elimu juu ya uwekezaji katika viwanda imetolea kwa wataalamu 3 wa kitengo cha  uwekezaji wakuu wa idara na vitengo vyote  na kamati ya fedha kupitia wataalamu wa EPZA

Timu hii ya uhamasishaji iliweza kufanya vikao vyake na kuwaeleza wananchi nia ya Serikali kutwaa ardhi ya kijiji kuwa chini ya kamishna kwa manufaa ya umma na jinsi wananchi hao watakavyo faidika kutokana na mradi huo wa EPZ kabla na baada kutwaa ardhi hiyo.

Vijiji ambavyo vipo kwenye eneo la mradi uwekezaji wa viwanda villikubaliana na mradi huo wa EPZ na kuomba haki zao za msingi zipatikane kwa muda muafaka na mhatasari huo uliwasilishwa ofisi ya ardhi wilaya. 

  • SEKTA YA MAENDELEO YA JAMII
  • Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ina Jumla ya Vikundi 150 vya wanawake vilivyo hai, ufuatiliaji ulifanyika katika vikundi 20 ambavyo vipo katika  kata za Mamaye, Idetemya, Misungwi, Mbarika, Buhingo, Misasi, Koromije, Usagara, na Ukiriguru. Vikundi kumi  vya wanawake vimepatiwa mkopo wenye thamani ya Tsh.31, 000,000.00 na Vikundi kumi  vya Vijana vimepatiwa mkopo wenye thamani ya Tsh.41, 600,000.00, ambapo Tshs.4,500,000.00 ni mchango wa Halmashauri na Tshs. 36,600,000.00 kutoka Serikali kuu. Shughuli nyingine zilizofanyika ni pamoja na jumla ya vikundi 56 vimesajiliwa,kati ya hivyo vikundi 21 tayari vimefungua Akaunti Benki, Vikundi sita (06) vimefanyiwa ufuatiliaji kwa lengo la kuhimiza marejesho ya mkopo. Jumla ya fedha zilizorejeshwa kutokana na mikopo ni Tsh. 4,133,000.00. Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ina jumla ya watoto waishio katika mazingira hatarishi na Yatima 12,390. Idadi ya watoto waishio katika mazingira hatarishi na yatima waliohudumiwa ni 4,384, ambapo Me ni 2,348 na ke ni 2,036. Huduma zilizotolewa ni pamoja na chakula, msaada wa kisheria, Afya, Elimu, makazi, matunzo na msaada wa kisaikolojia. Jumla ya vikundi viwili (02) vya vijana vimefanyiwa uhakiki. Vikundi hivyo ni Vijana Kwanza Usagara na Umoja wa Waendesha Pikipiki Misungwi, vikundi vine (04) vimepatiwa mkopo wenye thamani ya Tsh. 20,000,000.00 na Vikundi sita (06) vilivyopo katika kata ya Misungwi, Igokelo, Buhingo, Misasi, Koromije na Mbarika vimehakikiwa kwa lengo la kuvipatia mkopo.

15.0 SEKTA YA MIUNDOMBINU

15.1   SEKTA YA MIUNDO MBINU

Mtandao wa barabara umegawanyika katika sehemu kuu mbili, nazo  ni

Mtandao wa barabara Wilayani zilizo chini ya Mkoa, ambazo zipo katika mafungu mawili;-

Barabara za Taifa (Trunk Roads)               -             53 Km 

Barabara ya Mkoa (Region Roads)           -           167 Km

                                                            Jumla                         -           220 Km 

(b)  Mtandao wa barabara zilizo chini ya Halmashauri nazo ziko mafungu mawili;- 

  • Barabara za  wilaya (District Roads)         -           315.8 Km
  • Barabara  za vijiji (Village Roads)             -           387.7  Km 

                                    Jumla  kuu barabara zote  ni         -           704  Km

15.2 Hali ya barabara wilayani

Hali ya  barabara  zilizo  chini  ya Halmashauri tangu  Januari  2006  hadi  June  2016  ni  kama  ifuatavyo:-

  • Barabara za Changarawe  ambazo  zinapitika  mwaka mzima  ni   Km 192
  • Barabara  za  udongo  ambazo  zinapitika wakati  wa kiangazi  ni  Km 345.8

15.3 Changamoto 

Changamoto iliyopo  kubwa  ni ya uhaba wa fedha kulingana na mahitaji halisi. Hii imesababisha;

  • Barabara nyingi  kukosa Kalveti  za  kutosha  na  kujengwa madaraja  ya  mbao  mbayo  yanahitaji  matengenezo  baada ya muda mfupi
  • Barabara kutopitika kwa muda wote  kwa sababu  ya  kutowekewa changalawe 

15.4 Jinsi ya kukabili changamoto

Tumeweza kuomba fedha za nyongeza nje ya bajeti toka mfuko wa barabara.

Jedwali Na.14:  MGAWO WA FEDHA ZA BARABARA 2014/2015 NA 2015/2016 NA 2016/2017:

 
TAASISI
BAJETI YA FEDHA ZA BARABARA 2014/ 2015 (Tshs: )
BAJETI YA FEDHA ZA BARABARA 2015/ 2016 (Tshs: )
BAJETI YA FEDHA ZA BARABARA 2016/ 2017 (Tshs: )
 
 
JUMLA 
Misungwi
     914,300,000
391,300,000
882,220,000
2,187820,000
JUMLA KUU
     914,300,000
391,300,000
882,220,000
2,187820,000

 

15.5     VIVUKO:

Wilaya ya Misungwi haina miundo mbinu ya vivuko inavyovisimamia, kivuko kilichopo kinasimamiwa na mamlaka nyingine ambayo ni TEMESA

HUDUMA ZA KIJAMII

16 .0    SEKTA YA ELIMU:

 

16.1     Elimu ya Msingi

 

Jedwali Na.15: IDADI YA SHULE ZA AWALI NA MSINGI – KIWILAYA, 2016:

WILAYA
SHULE ZA AWALI
SHULE ZA MSINGI
Serikali
Binafsi
Jumla
Serikali
Binafsi
Jumla
Misungwi
138
7
145
138
7
145
JUMLA
138
7
145
138
7
145

Jedwali Na.16 : IDADI YA SHULE ZA MSINGI NA WANAFUNZI:  2016

AWALI – DARASA LA KWANZA

Na
WILAYA
IDADI YA SHULE
IDADI YA WANAFUNZI
Serikali
Binafsi
Jumla
Wav
Was
Jumla
1
Misungwi
138
7
145
42,949
34,525
67,474

JUMLA
138
7
145
42,949
34,525
67,474

 

Jedwali Na.17: Uandikishaji wa Darasa la Kwanza 2016:

NA

WILAYA

IDADI YA WANAFUNZI

WAV

WAS

JUMLA

1
Misungwi

9,590

9,264

18,854


JUMLA

9,590

9,264

18,854

 

Jedwali Na.18: IDADI YA WANAFUNZI DARASA LA I HADI VII - 2016

NA

WILAYA

IDADI YA WANAFUNZI
 
WAV
WAS
JUML

4

Misungwi

Serikali

35,977

37,463

73,440



Binafsi

524

513

1,037


JUMLA

 

36,501

37,976

74,477


 Jedwali Na.19:  TAKWIMU ZA WATAHINIWA WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI 2015 NA 2016 NA KUFAULU KUINGIA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2016 NA  2017  WILAYA YA MISUNGWI, MKOA WA MWANZA

NA
 
MWAKA
 

WALIOFANYA

WALIOFAULU

WAV
WAS
JML
WAV
%
WAS
%
JML
%
1
2015

2,474

2,921

5,395

1,991

80

2,199

75.3

4,190

77.7

2
2016

2,801

3,291

6,092

2,118

75.64

2064

62.71

4,182

68.65













                       

    Jedwali Na.  20: SAMANI ZA SHULE ZA MSINGI HADI DESEMBA 2016 

WILAYA

MADAWATI

MEZA ZA WALIMU

VITI VYA WALIMU

KABATI ZA WALIMU

MISUNGWI 
Mahitaji 
Yaliyopo 
Upungufu/Ziada 
Mahitaji 
Yaliyopo 
Upungufu 
Mahitaji 
Yaliyopo 
Upungufu 
Mahitaji 
Yaliyopo 
Upungufu 
JUMLA
34,597
35,132
535
3,178
1,087
2,091
3,504
1,366
2,138
1,906
411
1,495

  


 

16.2 Idadi ya walimu katika Shule za Msingi hadi Desemba 2016:

16.2.1 Idadi ya walimu na upungufu:

Jedwali Na.21:    MAHITAJI YA WALIMU HADI DESEMBA 2016  
 

NA

WILAYA

MAHITAJI

WALIOPO

UPUNGUFU

3
Misungwi
2,298
1,492
806

JUMLA
2,298
1,492
806

 

            Jedwali Na.22: MAHITAJI YA MAJENGO YALIYOPO NA UPUNGUFU KATIKA SHULE ZA MSINGI: HADI DESEMBA 2016

 

WILAYA

MADARASA

NYUMBA ZA WALIMU

VYOO

MAH

YAL

UPUNGUFU

MAH

ZILI

UPUNGUFU

MAH

YAL

UP

Misungwi
1,921
1,045
876
1,558
377
1,181
3,445
1,129
2,316
JUMLA
1,921
1,045
876
1,558
377
1,181
3,445
1,129
2,316

                                                              


17.0 ELIMU YA SEKONDARI

 

Jedwali Na.23:  IDADI YA SHULE ZA SEKONDARI ZENYE KIDATO CHA I-IV HADI DESEMBA 2016
                     
WILAYA
SERIKALI
ZISIZO ZA SERIKALI
JUMLA
Misungwi

23

04

27

JUMLA

23

04

27

 

 
Jedwali Na.24: SHULE ZENYE KIDATO CHA V-VI
 
WILAYA
SERIKALI
ZISIZO ZA SERIKALI
JUMLA
Misungwi

01

-

01

JUMLA:

01

-

01

 

Jedwali Na.25:  MAHITAJI YA WALIMU, WALIOPO NA UPUNGUFU HADI DESEMBA 2016

WILAYA

MASOMO YA SANAA

MASOMO YA SAYANSI

MAHITAJI

WALIOPO

UPUNGUFU

MAHITAJI

WALIOPO

UPUNGUFU

Misungwi
252
442
+190
220
104
116
JUMLA
252
442
+190
220
104
116

    

 

 

 

Jedwali Na. 26: SAMANI ZA SHULE ZA SEKONDARI,  HADI DESEMBA 2016 

WILAYA

MADAWATI

MEZA ZA WALIMU

VITI VYA WALIMU

KABATI ZA WALIMU

MISUNGWI 
Mahitaji 
Yaliyopo 
Upungufu/Ziada 
Mahitaji 
Yaliyopo 
Upungufu 
Mahitaji 
Yaliyopo 
Upungufu 
Mahitaji 
Yaliyopo 
Upungufu 
JUMLA
9,164
9,274
110
615
252
363
687
311
376
312
70
242

  

 

Jedwali Na.27:   IDADI YA MAJENGO  KATIKA SHULE ZA SEKONDARI:

 
WILAYA
 
MAKTABA
UTAWALA
KUMBI
HOSTEL/BWENI
MAH
YAL
UP
MAH
YAL
UP
MAH
YAL
UP
MAH
YAL
UP
Misungwi
23
0
23
23
19
4
23
01
22
23
01
22
JUMLA
23
0
23
23
19
4
23
01
22
23
01
22

 


17.1 CHANGAMOTO ZINAZOJITOKEZA KATIKA SEKTA YA ELIMU WILAYANI:

Ongezeko kubwa la wanafunzi ukilinganisha na uwiano wa walimu na miundombinu ya kufundishia na kujifunzia.

Kutokuwa na vitabu maalum/teule vya kiada kutokana na soko huria la vitabu

Upungufu wa walimu hasa walimu wa sayansi na hesabu

Ukosefu wa hostel, husababisha  watoto kupanga mitaani na hivyo kusababisha kupata mimba kwa watoto wa kike na kushindwa kumaliza masomo yao

Baadhi ya wanafunzi hutembea mwendo mrefu kwenda shuleni, hufika wamechelewa na wamechoka na kushindwa kufuatilia masomo

Ukosefu wa nyumba za walimu unasababisha walimu kuishi mbali na shule

Ukosefu wa Library za kutunzia vitabu na kusomea

Utoro wa wanafunzi

Ukosefu wa vitabu vya masomo ya sanaa (Art subjects)

Madeni ya malimbikizo ya mishahara baada ya kupandishwa kwa baadhi ya walimu.

 Wazazi kutofuatilia maendeleo ya watoto wao

Ukosefu wa chakula shuleni husababisha wanafunzi kushinda njaa na kushindwa kufuatilia masomo vizuri

Ukosefu wa vifaa vya maabara hasa yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi.

17.2 MIKAKATI YA UBORESHAJI WA ELIMU:

Kufanya ufuatiliaji mashuleni na kuhakikisha walimu waliopo    wanawasimamia wanafunzi ipasavyo.

Kushiriki vikao vya WDC ili kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo mashuleni, mfano; Utengenezaji wa madarasa na Ukarabati wa miundombinu ya shule.

Kutoa maelekezo kwa watendaji wa Kata kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi na kuwachukulia hatua wazazi wanaoendekeza utoro mashuleni.

Kuendesha vikao kwa wakuu wa shule na waratibu Elimu Kata ili kuwajengea uwezo wa kusimamia shule zao kwa ubora zaidi.

Halmashauri kuwashirikisha wadau mbalimbali katika shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Hostel kwa wanafunzi wa kike.

Wilaya inaendelea kuhamasisha wazazi kufuatilia maendeleo ya watoto wao ili kuwaandaa kufanya vizuri mitihani yao ya mwisho.

18.0     SEKTA YA AFYA:         

 18.1    AFYA YA MSINGI:

Lengo la afya ya msingi ni kuelekeza huduma za kinga na tiba karibu na wananchi kwa kushirikisha jamii, hadi sasa Wilaya imeweza kupanua huduma toka vituo 41 vya kutolea huduma za afya hadi kufikia vituo 46,  ambayo ni sawa na asilimia 39 ukilinganisha na vijiji 113 vilivyopo. Pia kuna ujenzi unaendelea wa Zahanati za Mapilinga, Mwamaguha na Ng’obo na ujenzi huu umefikia hatua ya ukamilishaji na ujenzi wa Zahanati ya Nyang’homango ujenzi upo katika hatua za ukamilishaji.

Halmashauri imeweza kupanua kituo cha afya cha Misasi kwa kujenga chumba cha upasuaji ili kuboresha afya ya uzazi,.pia bado ina mpango wa kupanua vituo vya Afya vya Busongo, Mbarika na Koromije ili viweze kutoa huduma ya upasuaji.

18.2     AFYA YA UZAZI NA MTOTO:

Huduma ya Uzazi na mtoto inatolewa kwenye vituo 46 vya kutolea huduma za Afya.

Akina mama wajawazito wanaojifungulia katika vituo vya Afya wameongezeka kutoka 72.1% kwa mwaka 2014 hadi 74.3% kwa mwaka 2015/2016.

Kiwango cha chanjo kwa watoto hadi Desemba 2016, kimepanda kufikia 91% (2015/16), matarajio kwa mwaka 2016/17 ni 120%.

18.3     UKIMWI:

UKIMWI bado ni tatizo kubwa katika wilaya ya Misungwi ingawa ukali wake umeendelea kupungua mwaka hadi mwaka, maambukizo kwa kigezo cha waliopima kwa hiari ni yameshuka kutoka asilimia 6.8 hadi 4.2 hii imetokana na uelewa wajamii kuhusu VVU na UKIMWI ,ingawa bado kuna unyanyapaa miongoni mwa Jamii zetu,kwa pamoja tumeweza kufikia vikundi 30 vya watu waishio kwa matumaini,NGO’s tatu (3) na vikundi 12 vinavyotoa msaada kwa watoto yatima walioko shule za msingi na NGO moja (1) inafanya kazi ya kudhibiti maambukizi mapya ya VVU.

.Mwaka 2016 kulikuwa na watu 10,457 waliojitokeza kwenye upimaji wa hiari na kati ya hao watu 1,105 sawa na asilimia 10.6 ya waliojitokeza walikutwa na maambukizo ya Virus vya UKIMWI (VVU). Wakati huu mpango wa dawa za kupunguza makali ya VVU/UKIMWI upo, hivyo watumiaji wa dawa hizo wapo. Kwa kipindi cha miaka 11 iliyopita waliojiandikisha kwa ajili ya kupata dawa za kupunguza makali ya VVU/UKIMWI ni watu 10,725 na walio katika matumizi ya dawa ni 4, 446 tu.

18.4     MALARIA:

Malaria ni ugonjwa ambao bado unaongoza kwa wagonjwa wengi wanaopata huduma za matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya. Jumla ya wagonjwa 45,452 walitibiwa kama wateja wa nje na jumla ya wagonjwa 4,112 walilazwa kwa tatizo la malaria kali (severe Maralia)

Katika swala la kupambana na Malaria Idara ya Afya inafanya shughuli zifuatazo;-

Kutoa tiba sahihi kwa wagonjwa wanaopatikana na vimelea vya ugonjwa wa Malaria baada ya kupima kwa kutumia vipimo vya MRDT.

Ugawaji wa vyandarua kwa akina mama wajawazito wanaohudhuria clinic kwa hudhurio la kwanza pamoja na watoto wa umri wa miezi tisa (9) wanaoenda kupata chanjo ya Surua, zoezi hili linafanyika kwenye vituo vyote vya kutolea huduma.

Utoaji wa Elimu ya Afya juu ya kujikinga na ugonjwa wa Malaria kwa jamii, kazi hii inafanywa na wahudumu wa Afya ya Jamii waliopata mafunzo ambao wapo kila Kata.

Kuhakikisha kunakua na upatikanaji wa vitenganishi na dawa kwa ajili ya Malaria.

Ugawaji wa vyandarua 19,154 viligawiwa kwenye Jamii kupitia wanafunzi wa darasa la kwanza kwenye shule za msingi zote Wilayani.

18.5     UPATIKANAJI WA DAWA NA VIFAA VYA TIBA KWENYE VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA:

Dawa na vifaa tiba hupatikana kutoka vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Bohari ya dawa Mwanza (MSD) na toka Fedha ya Mfuko wa Afya ya pamoja (Hearth Busket Fund). Dawa ambazo hutolewa na MSD zimepatikana kwa asilimia 87.13 na dawa ambazo tunanunua kupitia Mfuko wa Afya wa pamoja  hununuliwa kwa asilimia 100.

18.6 CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI SEKTA YA AFYA WILAYANI:

Uchakavu wa miundombinu ikiwemo majengo ya OPD na nyumba za watumishi.

Uchakavu na upungufu wa vyombo vya usafiri ususani Ambulance.

Upungufu wa watumishi wa fani mbalimbali kulingana na ikama halisi kama kada za Madaktari, Mionzi, Maabara, Wazoeza viungo, Macho,Pua na Koo

Ufinyu wa bajeti kulingana na gharama halisi za utoaji huduma za afya

Ukosefu wa vitendea kazi ikiwemo dawa na vifaa tiba toka bohari ya dawa Mwanza (MSD)

Mwamko mdogo wa Jamii kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)

18.7 Mikakati ya Kukabiliana na Changamoto:

  • Wilaya inaendelea na ukarabati wa miundombinu kwa kutumia fursa zilizopo kama Malipo kwa Ufanisi (RBF), Nguvu za wananchi na MMAM.
  • Wilaya kuweka kwenye bajeti maombi ya watumishi wa kada mbalimbali katika Idara ya Afya.
  • Wilaya inaendelea kuboresha vyanzo vingine vya upatikanaji wa fedha kwa kutumia fursa zilipo na kupitia vyanzo vifuatavyo, mfuko wa afya ya Jamii (CHF), Michango ya papo kwa papo (Cost sharing) na Bima ya Taifa ya Afya (NHIF)
  • Wilaya kwa kushirikiana na jamii husika inakarabati na kujenga nyumba za watumishi. Pia jitihada za kutafuta wafadhili wa kuweza kufadhili ujenzi na ukarabati wa Hospitali ya Wilaya zinaendelea kufanyika.
  • Uhamasishaji ngazi ya vijiji/Kata na kwenye mikutano ya hadhara unaendelea kufanyika ili kuhamasisha jamii kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).

19.0 USTAWI WA JAMII

19.1     HUDUMA KWA WAZEE:

Halmashauri ya Wilaya ina jumla ya wazee 12,360, kati ya hao wanaume ni 5,982 na wanawake 6,378.kundi hili linapewa huduma za matibabu kwa msamaha. Wazee 2,910

( Me 1,358 na Ke 1,552) wametambuliwa katika Kata za Mbarika, Kasololo, Misasi na Usagara na kupatiwa vitambulisho vya msamaha wa matibabu. Vituo vyote vya tiba vinatoa huduma kwa wazee bila Malipo. Katika Hospitali ya Wilaya wazee wanatibiwa katika chumba maalumu.

19.2 WATU WENYE ULEMAVU:

Wilaya ya Misungwi ina jumla ya walemavu 1523 ambapo kati ya hao wanaume ni 731 na wanawake ni 792.Aidha  idadi ya walemavu wa ngozi ( albino)  katika Wilaya ya Misungwi ni 137 kati ya hao wanaume ni 64  na wanawake 73.Ili kupiga vita mauaji ya albino mambo yafuatayo yamezingatiwa, kuwatambua albino, kufahamu sehemu wanazoishi na kufanya uchaguzi wa uongozi wao kiwilaya. Uchaguzi ulifanyika mwaka 2015 uhamasishaji kwa jamii umefanyika walindwe chini ya usimamizi wa viongozi wa familia na Uongozi wa Serikali ya  vijiji na Kata. Katika Wilaya ya Misungwi idadi ya albino waliouwawa ni 3 tangu mwaka 2007 mpaka sasa. Aidha Wilaya yetu ina shule moja ya msingi ya Mitindo yenye kitengo maalum kwa ajili ya walemavu wakiwemo wa ngozi (Albino). Shule hiyo ina walemavu wa ngozi (Albino) wapatao  91  kati yao wavulana ni  39 na wasichana ni 52 kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Mwanza.

 19.3   MAPAMBANO DHIDI YA MAUAJI YA ALBINO:

Wilaya baada ya kuwajengea uwezo wananchi juu ya athari za mauaji ya Albino, hivi sasa wananchi wamekuwa na uelewa mkubwa hivyo mauaji yamepungua kwa kiwango kikubwa.

19.4   WATOTO WALIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI:

Mpango wa kutambua na kuelimisha jamii juu ya matunzo ya watoto waishio katika mazingira hatarishi umetekelezwa katika kata 14 kati ya kata 27 na vijiji 54 kati ya vijiji  113. Jumla ya watoto 7,412 wametambuliwa kati yao 3,842 wa kiume na 3,570 wa kike. Baada ya utambuzi huo jumla ya kamati 54 za watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ziliundwa. Zoezi hili la utambuzi lilifanywa na shirika la MOCSO.

20.0     SEKTA YA MAJI

21.1 MAJI MJINI

21.1.1 TAARIFA YA HALI HALISI YA UTOAJI WA HUDUMA YA MAJI MJINI MISUNGWI.

Mamlaka ya Maji Mjini Misungwi ni kati ya Mamlaka 5 za makao makuu ya Wilaya katika Mkoa wa Mwanza. Mamlaka ilianzishwa kwa mujibu wa Sheria Na. 8 ya mwaka 1997 ambayo imerekebishwa na Sheria Na. 12 ya mwaka 2002.

Mamlaka ina jumla ya Wateja wapatao 1402 katika makundi ya fuatayo:

Maji manyumbani               -           1308.

Maji Biashara                        -           38

 Maji Taasisi                          -           44

Magati ya kuchotea Maji    -           12

Mji wa Misungwi una jumla ya watu/wakazi wapatao 41,224, idadi hii inajumlisha vitongoji vya Mwambola, Mapilinga, Nange, Mwajombo, Iteja na Misungwi yenyewe.  Mahitaji ya maji yanakisiwa kuwa meta za ujazo 3273 kwa siku, wakati uzalishaji toka chanzo cha Nyahiti (Ziwa Victoria) ni meta za ujazo 600 kwa siku (600m3/Day) sawa na asilimia 18 ya mahitaji ya Jumla ya watu wapatao 21,000 wanaopata huduma ya maji.

Kuna jumla ya miradi miwili ambayo ni Nyahiti intake (Chanzo ni Ziwa Victoria) na Mitindo dam (Bwawa la Mitindo) na yote yanafanya kazi.

21.2 Usambazaji wa maji Mjini (Mitindo Water Supply):

Ni mradi uliokuwa ukihudumia wakazi wa mji wa Misungwi, baada ya mradi toka ziwa Victoria kukamilika ulibaki kuwa wa dharura. Mradi wa mitindo una mabwawa madogo matatu ya kuhifadhi maji(Three Storage Tanks) yenye ujazo tofauti  yaani 50m3,30m3 na 12m3 na yana uwezo wa kuhifadhi jumla ya Meta za ujazo tisini na Mbili (92m3).

21.4 Changamoto:

Upatikanaji wa maji haulingani na mahitaji ya wakazi wa Mji wa Misungwi kwa sababu zifuatazo:-

  • Bomba kuu (Main Transmission Line) kutoka Nyahiti lenye urefu wa 12.5km ambapo 2.5 Km ni kuukuu sana na husababisha upotevu wa maji kutokana na Matengenezo ya mara kwa mara. 
  • Mtandao wa kusambaza maji (distribution network) unaotumika ni wa zamani ambayo una jumla 27 km.
  • Tanki linalotumika sasa ni dogo (meta za ujazo 225) na ni Tanki pekee linalopokea Maji kutoka Nyahiti ambapo bomba kuu linaloleta maji kwenye Tanki kutoka chanzo cha Nyahiti lina kipenyo cha 8” (8 inch) wakati linalosambaza maji kutoka kwenye Tanki kwenda kwa wateja lina Kipenyo cha 4”.
  • Maji yanayotolewa hayakidhi viwango vinavyokubalika Kimataifu kwa sababu hakuna mtambo wa kuchujia na kutibia maji (treatment plant).

21.5 Namna ya kutatua changamoto hizi (The wayforward).

  • Kujenga tanki kubwa linalolingana na mahitaji ya sasa.
  • Kupanua na kuongeza mtandao wa kusambaza maji.
  • Kujenga chanzo kipya kinachokidhi mahitaji ya sasa.
  • Kujenga mtambo wa kutibia maji.
  • Kuanzisha huduma ya maji taka kwa kujenga mabwawa ya kutibia maji machafu (feacal sludge ponds).

Yote haya yanatarajia kutekelezwa kupitia mradi mkubwa wa kuboresha miundo mbinu ya maji kwa miji ya Misungwi, Magu, Lamad, Bukoba, Musoma na Mwanza na, unaofadhiliwa na Benki ya uwekezaji ya Ulaya (EUroppean Investment Bank) (EIB) na Shirika la maendeleo la Ufaransa (AFD - Agency for French Development).

 

22.0 MAJI VIJIJINI

Lengo kuu la sekta ya maji ni kuhakikisha kwamba wananchi wa Misungwi wanapata huduma ya maji safi na salama kwa gharama nafuu mita 400 kutoka kwenye chanzo hadi kwenye kaya .Idadi ya watu wanaopata huduma yamaji safi na salama vijijini na mjini ni 150,565 ambayo ni sawa na asilimia 43 ya jumla ya watu 351,607 waliopo wilayani.

22.1 MIRADI YA MAENDELEO PROGRAMU YA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI (RWSSP)

Katika mwaka huu wa fedha 2016/2017 Halmashauri kupitia Idara ya Maji imepanga kukamilisha ujenzi wa  miradi mitatu ya Maji bomba katika vijiji vya Igenge,Ngaya- Matale,Matale –Manawa – Misasi kupitia Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RWSSP) chini ya usimamizi wa Mhandisi Mshauri COWI Tanzania na usimamizi wa ndani kupitia Halmashauri na Secretarieti ya Mkoa.

22.2 Mchanganuo wa Miradi ya maendeleo;-

a) Ujenzi wa Mradi wa Maji bomba Igenge

Mradi huu unajengwa na Mkandarasi aitwaye Seekevim Ltd wa Dar-es salaamu.  Shughuli zilizopangwa kutekelezwa kwa mujibu wa mkataba ni: 

  • Kujenga tanki la maji lenye ujazo wa 135m3
  • Kujenga njia ya mtandao wa maji kijijini km 19
  • Kujenga sehemu za  watu kuchotea maji DPs 11
  • Kujenga birika 3  za kunyweshea mifugo( cattle Trough )
  • Kujenga tanki la kuvuna maji ya mvua shule ya msingi Igenge  lenye ujazo wa 5m3
  • Kufunga dira za maji 16

 

22.3 Hali ya utekelezaji kufikia Septemba 30 2016 ni kama ifuatavyo:-

  • Tanki la maji lenye ujazo wa 135m3 limejengwa bado tu halijafunikwa
  • Mabomba yameungwa na kulazwa urefu wa km 15 .
  • Tanki  la kuvuna maji ya mvua lenye ujazo wa lita 5000 limejengwa shule ya msingi Igenge bado kufunga “Gutter”
  • Maeneo yote 11  ya kuchotea maji (DPs) yameshajengwa pamoja na chemba zake
  • Mtaro wa km 15 umeshachimbwa kwa ajili ya kulaza mabomba
  • Birika 3 za kunyweshea mifugo zimejengwa na kukamilika.
    •  
    • 22.4 Ujenzi wa Mradi wa Maji bomba wa Ngaya hadi Matale.
  • Mradi huu unajengwa na mkandarasi aitwaye CMG Construction Co.Ltd wa jijini mwanza. Shughuli zilizopangwa kutekelezwa kwa mujibu wa mkataba ni:-


    •  Kujenga njia ya mtandao wa maji kijijini km13.292
    •  Kujenga sehemu za  watu kuchotea maji DPs 10,
    •  Kukarabati tanki lenye ujazo wa 45m3
    •  Kujenga chemba 10
    •  Kufunga dira za maji 10
  • 22.5 Hali ya utekelezaji kwa sasa ni kama ifuatavyo.


    •  Tanki lenye ujazo wa 45m3 limekarabatiwa asilimia 90.
    •  Mkandarasi amejenga mtandao wa kusambaza Maji km 10 toka Ngaya hadi Sumbugu.
    •  Maeneo yote 10 ya kuchotea maji (DPs) yameshajengwa pamoja na chemba zake .
      • Ujenzi wa Mradi wa Maji bomba wa Matale –Manawa-Misasi
    • Mradi huu unajengwa na mkandarasi aitwaye Syscon Builders Construction Ltd wa Dar-es-salaam. Shughuli zilizopangwa kutekelezwa kwa mujibu wa mkataba ni:-


      • Kujenga njia ya mtandao wa maji kijijini km14
      •  Kujenga sehemu za  watu kuchotea maji DPs 19,
      •  Kujenga  tanki lenye ujazo wa 135m3
      •  Kujenga chemba 15
      •  Kufunga dira za maji 20
    • 22.7 Hali ya utekelezaji kwa sasa ni kama ifuatavyo:-


      • Mkandarasi ameandaa matofali kwa ajili ya kujenga tanki la ujazo wa 135m3
      • Mkandarasi amejenga mtandao wa kusambaza maji km 11 toka Matale
      • Amejenga maeneo yote 19 ya kuchotea maji (DPs) na chemba zake.
    • 22.8 Changamoto za Idara katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo

       
       
       
       
       
       
      Jedwali Na.28.: Wastani wa Utoaji wa Huduma ya Maji safi Wilayani

      Wilaya

      Idadi ya Vijiji

      Idadi ya watu

      Idadi ya watu wanaopatiwa huduma ya maji

      Kiwango cha asilimia

      Misungwi
      113
      351,607
      150,565
      43

      • Kuchelewa kwa kutolewa fedha kumesababisha miradi kushindwa kukamilika kwa wakati.
      • Ukosefu wa Wataalamu wa kada ya Uhandisi wa Rasilimali Maji.
        • 22.9 Utatuzi wa Changamoto 
      • Wizara ya Maji ilete fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wakati ili miradi iweze kukamilika na kutoa huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.
      • Wizara iajiri watumishi ili kuziba pengo la uhaba wa watumishi


23. 0 HALI YA UTUMISHI KATIKA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

23.1     HALI YA UTUMISHI:

Hali ya utumishi katika Halmashauri ya wilaya ya Misungwi ni kama ilivyo katika Halmashauri zingine, tunakumbwa na uhaba mkubwa katika kada za Afya, Elimu na Kilimo. Kwa ujumla Halmashauri ina watumishi wapatao 3,011 kati ya mahitaji halisi ya 4,214  hivyo kufanya upungufu wa watumishi kufikia1,203. Aidha tunaendelea na mpango wa kuhakikisha kuwa nyumba za watumishi zinajengwa ili kuhakikisha kuwa watumishi hao wanapata mazingira mazuri ya kufanyia kazi. Hadi sasa Halmashauri imeshajenga nyumba 11 za watumishi wa Halmashauri. Bado tunaomba Serikali kuendelea kutusaidia kujenga nyumba zingine  zaidi ili kuweza kukidhi mahitaji ya watumishi.

23.2 UPANDISHWAJI VYEO:

  • Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2015/2016 imeweza kuwapandisha watumishi wa kada mbalimbali kutoka idara ya afya, elimu, utawala, kilimo na mifugo wapatao 715.Hata hivyo upandishaji vyeo kwa watumishi wa umma  kwa sasa umesimama kutokana na Agizo la Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,DR John Joseph Pombe Magufuli.
  •  
  •  23.3 CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI SEKTA YA UTUMISHI:
  • Wilaya inaupungufu wa raslimali fedha kwa ajili ya kutoa mafunzo nje na ndani katika kupanua wigo wa ujuzi na weledi katika kazi na vitendea kazi vinavyoendana na wakati (Science and technolodge).
  • Aidha Idara ina kabiliwa na tatizo kubwa la Madeni ya watumishi, ikiwemo uhamisho, likizo na malimbikizo ya Mishahara.
  • Pia Wilaya ina upungufu wa watumishi (wataalamu) katika kada mbalimbali hasa elimu msingi.
  • Wilaya ina upungufu wa nyumba za watumishi hasa watumishi wanaofanya kazi ngazi za vijiji na kata.

23.4 TAARIFA YA UHAKIKI WA WATUMISHI

Serikali kwa kupitia Vyombo/Taasisi mbalimbali, imefanikiwa kufanya Uhakiki wa watumishi kwa kuangalia Taaluma zao, aidha watumishi wachache wameweza kubainika kujipatia ajira kwa udanganifu na wengine kutowajibika ipasavyo. Hali hii imepelekea Mamlaka za kinidhamu kuwafukuza na wengine kuchukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu.

24.0     Huduma za Fedha Zinazotolewa na Taasisi mbalimbali

Wilaya ya Misungwi inazo Benki mbili za NMB na CRDB zinayotoa huduma kwa wananchi wake. Pia kuna SACCOS ya MKUKUWAMI ambayo hutoa mikopo kwa wanachama wake na Taasisi za kifedha kama Maboto ,Bayport,Equity,Faidika

25.0 Mawasiliano

Wilaya ya Misungwi imebahatika kuwa na mitandao ya simu kutoka katika makampuni ya simu mbalimbali na kuwafanya wananchi wake kuweza kuwasiliana na ndugu na jamaa zao katika kuboresha mahusiano ya kijamii na kibiashara. Makampuni ya simu yanayotoa huduma za simu ni kama ifuatavyo; Kampuni za Vodacom, Tigo, Airtel, TTCL, Halotel na Zantel.  Aidha bado kuna changamoto katika maeneo mengi ya vijijini ambako makampuni hayo bado hayajaweka minara yao ili kuongeza mtandao wa huduma hizo.

26.0     Hitimisho

Wilaya inatoa shukrani kwa Serikali yetu kwa kuiwezesha Jamii kupata miradi ya maendeleo ambayo itatoa matokeo ya muda mfupi na haraka “Big Results Now –BRN” na imechangia kuboresha miundo mbinu mjini na vijijini, ambayo itaboresha hali ya maisha kwa kuongeza vipato kwa walengwa.

Naomba kuwasilisha

JUMA S. SWEDA

MKUU WA WILAYA

MISUNGWI

Matangazo

  • SHULE ZILIZOVUNJA REKODI KATIKA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2024 February 01, 2025
  • TANGAZO ZABUNI UPANGISHAJI VIBANDA VYA HALMASHAURI MWAKA 2023/2024 June 28, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 20, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE WA JIMBO LA MBARALI NA MADIWANI KATIKA KATA SITA ZA TANZANIA August 10, 2023
  • Angalia yote

Habari Mpya

  • DC Misungwi awataka Wananchi wa Kijiji cha Ibinza kata ya Isenengeja kudumisha amani na mshikamano.

    May 22, 2025
  • DC Misungwi akabidhi Vifaa saidizi vya Vitimwendo 15, Jezi na Mipira kwa Wanafunzi na Watoto wenye ulemavu kukwa Shule za msingi 16.

    May 21, 2025
  • Misungwi yapongeza kwa upatikanaji wa Mitambo ya kuondoa magugu maji itakayowasili mwishoni mwa mwezi julai 2025

    May 19, 2025
  • DC Misungwi awapongeza Waalimu wa Shule za Sekondari kwa ufaulu wa Asilimia 99.75

    May 16, 2025
  • Angalia yote

Video

Uzinduzi wa Tovuti za Mikoa pamoja na Halmashauri
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Takwimu za wanafunzi kitaifa
  • Taarifa
  • Kujisajili chama cha Mapinduzi-ccm
  • MFUMO WA UJAZAJI MATAMKO KWA NJIA YA MTANDAO
  • KUPATA KIUNGANISHI CHA MFUMO WA TAARIFA ZA SHULE-SIS
  • Historia ya Halmashauri
  • Sheria Mbalimbali
  • Wasiliana Nasi
  • Malalamiko

Viunganishi Linganishi

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tamisemi
  • Mwanza Region
  • Wakala wa Serikali Mtandao (Ega)

Ramani ya Wasomaji

world map hits counter

Wasomaji

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Misungwi

    Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI

    Simu ya Mezani: +255282983268

    Simu ya Mkononi: 0717259106

    Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.