Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt, Hussein Mwinyi akisisitiza jambo kuhusu ulipaji Fidia kwa Wananchi walio katika maeneo yanayochukuliwa na Jeshi la Wananchi katika Kitongoji cha Kirumba Kijiji cha Kigongo Wilayani MIsungwi, (katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,John Mongela pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Juma Sweda.(kushoto)
Mojawapo ya eneo lililopo Kandokando ya Ziwa Victoria linalotarajiwa kuchukuliwa kwa ajili ya matumizi ya Jeshi la Wananchi Tanzania katika Kitongoji cha Kirumba Kijiji cha Kigongo Wilayani Misungwi eneo ambalo linakadiriwa kuwa na Kaya zaidi ya 52.
Baadhi ya Wananchi wa Kitongoji cha Kirumba katika Kata ya Idetemya wakimsikiliza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa akizungumza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali kuhusu ulipaji wa Fidia katika eneo litakalotumiwa na Jeshi la Wananchi katika masuala ya kiusalama.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela akitoa salaam za Mkoa kwa Wanachi wa Kitongoji cha Kirumba Kijiji cha Kigongo Wilayani Misungwi,na amewataka Wananchi hao kuendelea na uvumilivu kama waliuonyesha kwa muda mrefu sasa kuhusu Fidia wakati Serikali inakamilisha taratibu za kisheria za uthamini wa maeneo hayo (kulia ) Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa ,Dkt, Hussein Mwinyi na (kushoto) ni Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Juma Sweda wakimsikiliza kwa makini.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt, Hussein Mwinyi akiwaeleza Wananchi wa Kijiji cha Kigongo Wilayani Misungwi kuhusu hatua ambazo Serikali imechukua na kuwaahidi Wananchi hao kwamba zoezi la uthamini litafanyika hivi karibuni ikiwa ni hatua za kisheria za ulipaji wa Fidia kwa wamiliki halali wa maeneo yatakayochukuliwa kwa matumizi ya Jeshi la Wananchi pamoja na ulinzi na usalama na miundombinu ya Daraja la Kigongo - Busisi lilioanza kujengwa na Serikali, (wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, juma Sweda.
Baadhi ya Eneo litakalochukuliwa kwa matumizi ya Jeshi la Wananchi lililopo katika Kitongoji cha Kirumba kwenye Kijiji cha Kigongo Kata ya Idetemya Wilayani Misungwi eneo ambalo Serikali imeahidi kufanya uthamini mapema ili Wananchi waweze kulipwa Fidia stahiki.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.