• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ardhi na Maliasili
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Maeneo ya Vivutio vya Utalii
    • Maeneo ya Kilimo
    • Maeneo ya Madini
    • Maeneo ya Uwekezaji wa Mazingira
  • Huduma Zetu
    • Huduma Sekta ya Afya
    • Huduma Sekta ya Elimu
    • Huduma Sekta ya Maji
    • Huduma Sekta ya Mazingira
    • Huduma Sekta ya Maendeleo ya Jamii
    • Huduma Sekta ya Ardhi na Maliasili
  • Baraza la Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Huduma za Kijamii
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba Vikao vya Halmashauri
  • Miradi mbalimbali
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Mbalimbali
    • Taratibu
    • Gazeti la Serikali
    • Taarifa
    • Fomu mbalimbali
    • Zabuni
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Video Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Habari Mpya

Watahiniwa 7,776 watarajiwa kufanya Mitihani ya kumaliza Elimu ya Msingi mwaka 2019 Wilayani Misungwi.

Imewekwa : September 10th, 2019

Jumla ya Watahiniwa 7,776  wanatarajiwa kufanya Mitihani ya kumaliza Elimu ya Msingi kuanzia tarehe 11 hadi 12 mwezi Septemba  mwaka 2019 katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.

Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Bw,  Frank Magabiro ameeleza haya kwa Waandishi wa Habari ofisini kwake mapema leo, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi,  Bw, Kisena Mabuba, alisema kwamba Halmashauri hiyo imeshafanya na kukamilisha  maandalizi yote ya zoezi la  kitaifa la uendeshaji wa Mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi kwa Wanafunzi wa darasa la saba mwaka 2019.

Bw, Magabiro amesema kwamba kuna jumla ya Watahiniwa 7,776 waliosajiliwa kwa ajili ya kufanya Mtihani huo wa kumaliza Elimu ya msingi kwa mwaka 2019, ambapo Wavulani ni 3,596 na Wasichana ni 4,180 na tayari maandalizi ya msingi na mambo mengine yapo vizuri hususani suala la usafiri na usambazaji wa Mitihani kuelekea katika Vituo 146.

Bw, Frank Magabiro Afisa Elimu Msingi, wa Halmashauri ya wilaya  ya Misungwi, akizungumza na Wanahabari ofisini kwake mapema jana, 

Mwl, Twaha Hussein Said ambaye ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mbela, akizungumza ofisini kwake na Bw, Frank Magabiro Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Misungwi, wakati alipotembelea Shuleni hapo kuona maandalizi ya msingi ya zoezi la Mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi inayotarajiwa kufanyika tarehe 11 na 12 mwezi Septemba 2019.

Bw, Magabiro alifafanua kuwa kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania inaeleza kwamba Mitihani hiyo ya kumaliza Elimu ya Msingi  itaanza siku ya Jumatano kuanzia saa 2.00 asubuhi kwa watahiniwa kufanya masomo ya English Language , Hisabati na Maarifa ya jamii na kukamilika siku ya Alhamisi kwa  Watahiniwa kufanya masomo ya Kiswahili na Sayansi.

Afisa Elimu huyo ameongeza kuwa kwa upande wa Watahiniwa wa Mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi mwaka huu 2019 kumekuwepo na ongezeko la Watahiniwa 188 ambayo ni sawa na asilimia 2.4 ya Watahiniwa 7,588 waliohitimu Elimu ya Msingi mwaka  jana 2018 katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.

Bw, Frank Magabiro amebainisha sababu iliyowezesha kuongezeka kwa Watahiniwa hao ni pamoja na udhibiti wa utoro kwa Wanafunzi, mwitikio wa  Wazazi na jamii katika suala la Elimu sambamba na utekelezaji wa Sera ya Serikali ya utoaji wa Elimu bila malipo ambayo inatekelezwa katika Shule zote  za msingi 147, zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi zikwemo Shule za Serikali 139 na shule binafsi 8.

Akizungumza kuhusu maandalizi ya Wanafunzi katika masomo, Bw, Magabiro alisema kwamba Wanafunzi wote wameendaliwa vizuri kimasomo ambapo mada zote zilizopaswa kufundishwa zote zilikamilishwa, na wamefanya majaribio ya kutosha pamoja  na Mitihani mbalimbali ya ngazi ya Kata, Wilaya sambamba na Mtihani wa MOCK Mkoa, pia wamejengwa vizuri kisaikolojia na Walimu pamoja na Wazazi ‘’ameongeza kuwa kimsingi Watahiniwa wote wapo tayari kufanya Mitihani hiyo’’. Alisisitiza  Bw, Magabiro.

Bw, Magabiro amewataka Watahiniwa hao kuwa watulivu na kutambua kwamba Mtihani huo wa Taifa ni sawa na Mitihani mingine na kuwatakia kheri na Afya njema wakati wote na kuwaomba wamtangulize Mungu awasaidie katika Mitihani hiyo muhimu.

Bw, Frank Magabiro Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Misungwi, akizungumza na baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbela katika Kata ya Misungwi, ambayo ina Watahiniwa 167 watakaofanya Mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi mwaka huu 2019, amewaasa na kuwatia moyo  na kuwatakia kheri katika Mitihani yao na kuwaomba kuwa waaminifu.

Matangazo

  • SHULE ZILIZOVUNJA REKODI KATIKA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2024 February 01, 2025
  • TANGAZO ZABUNI UPANGISHAJI VIBANDA VYA HALMASHAURI MWAKA 2023/2024 June 28, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 20, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE WA JIMBO LA MBARALI NA MADIWANI KATIKA KATA SITA ZA TANZANIA August 10, 2023
  • Angalia yote

Habari Mpya

  • DC Misungwi awataka Wananchi wa Kijiji cha Ibinza kata ya Isenengeja kudumisha amani na mshikamano.

    May 22, 2025
  • DC Misungwi akabidhi Vifaa saidizi vya Vitimwendo 15, Jezi na Mipira kwa Wanafunzi na Watoto wenye ulemavu kukwa Shule za msingi 16.

    May 21, 2025
  • Misungwi yapongeza kwa upatikanaji wa Mitambo ya kuondoa magugu maji itakayowasili mwishoni mwa mwezi julai 2025

    May 19, 2025
  • DC Misungwi awapongeza Waalimu wa Shule za Sekondari kwa ufaulu wa Asilimia 99.75

    May 16, 2025
  • Angalia yote

Video

Uzinduzi wa Tovuti za Mikoa pamoja na Halmashauri
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Takwimu za wanafunzi kitaifa
  • Taarifa
  • Kujisajili chama cha Mapinduzi-ccm
  • MFUMO WA UJAZAJI MATAMKO KWA NJIA YA MTANDAO
  • KUPATA KIUNGANISHI CHA MFUMO WA TAARIFA ZA SHULE-SIS
  • Historia ya Halmashauri
  • Sheria Mbalimbali
  • Wasiliana Nasi
  • Malalamiko

Viunganishi Linganishi

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tamisemi
  • Mwanza Region
  • Wakala wa Serikali Mtandao (Ega)

Ramani ya Wasomaji

world map hits counter

Wasomaji

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Misungwi

    Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI

    Simu ya Mezani: +255282983268

    Simu ya Mkononi: 0717259106

    Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.