• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Misungwi District Council
Misungwi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ardhi na Maliasili
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Maeneo ya Vivutio vya Utalii
    • Maeneo ya Kilimo
    • Maeneo ya Madini
    • Maeneo ya Uwekezaji wa Mazingira
  • Huduma Zetu
    • Huduma Sekta ya Afya
    • Huduma Sekta ya Elimu
    • Huduma Sekta ya Maji
    • Huduma Sekta ya Mazingira
    • Huduma Sekta ya Maendeleo ya Jamii
    • Huduma Sekta ya Ardhi na Maliasili
  • Baraza la Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Huduma za Kijamii
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba Vikao vya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Mbalimbali
    • Taratibu
    • Gazeti la Serikali
    • Taarifa
    • Fomu mbalimbali
    • Zabuni
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Video Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Habari Mpya

DC Misungwi aagiza Watendaji kukusanya Ushuru wa Madini ya Dhahabu na Almasi

Posted on: September 25th, 2018

MKUU WA WILAYA  AAGIZA  WATENDAJI WA HALMASHAURI KUKUSANYA  MAPATO YA USHURU WA MADINI YA DHAHABU NA ALMASI

Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe,Juma Sweda amewataka Watendaji wa Halmashauri kufuatilia na  kuhakikisha wanakusanya Mapato yanayotokana na Ushuru wa Huduma kutoka kwa Makampuni yanayofanya shughuli za Uchimbaji na Uchenjuaji wa Madini ya Dhahabu na Almasi katika Migodi iliyopo maeneo ya Ishokela na Mwanagwa Wilayani humu.

Akizungumza na Menejimenti ya Halmashauri mapema leo Mhe, Mkuu wa Wilaya ya Misungwi amewaagiza Wakuu wa Idara na Vitengo kuhakikisha kwamba Mapato hayo yanayotokana na Ushuru wa Huduma yanakusanywa kutoka  kwa Makampuni yote yanayojishughulisha na Uchimbaji na uchenjuaji wa Madini ya dhahabu na Almasi katika  maeneo mbalimbali kwa kipindi chote ambacho hawajalipa ili kuweza kuboresha na kuongeza Makusanyo ya Mapato ya ndani ya Halmashauri.

Mhe,Juma Sweda amesema kuwa Wamiliki wa Makampuni ya Uchimbaji na Uchenjuaji  yote yanayofanya kazi katika maeneo ya Ishokela, Mwamazengo, Shilalo, Mwanangwa na Mabuki yanapaswa kulipa Mapato ya Ushuru wa Huduma kwa Halmashauri wanapofanyia kazi na kwa mujibu wa takwimu zilizopo Makampuni hayo hayalipi kabisa na matokeo yake Halmashauri imepoteza Mapato hayo kwa muda mrefu sasa, na kuwataka Watendaji wafuatilie na kuhakikisha wote wanalipa Ushuru wa mwaka 2018/2019 pamoja na madeni yote ya nyuma.

Ameeleza kuwa ameweka Mikakati ya kuyafungia kufanya kazi ya Uchimbaji Makampuni ambayo yatashindwa kukamilisha malipo ya Ushuru husika na kuwaomba Wamiliki hao kulipa mapema vinginevyo hatua za Kisheria zitachukuliwa dhidi yao pamoja na kufungiwa kufanya shughuli za uchimbaji katika maeneo yote ya Wilaya ya Misungwi.

Mhe,Juma Sweda amewataka pia Watendaji wa Halmashauri ya Misungwi kufanya kazi kwa uaminifu, uadilifu wa hali ya juu pamoja kutekeleza majukumu yao kwa Weledi kwa lengo la kuleta ufanisi na kuongeza tija kazini hususan katika suala la kuongeza na kuimarisha ukusanyaji wa Mapato ya vyanzo vya ndani kwa njia ya Kielektroniki pamoja na kusimamia utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiliwa na Serikali na Wadau wengine kupitia Sekta ya Afya,  Elimu, Maji, Kilimo, Mifugo na Uvuvi, TASAF III, miundombinu na Maendeleo ya Jamii kwenye miradi ya Vikundi vya Wanawake ,Vijana na Wenye Ulemavu.

Ameagiza Wakuu wa Idara na Vitengo kwenda Vijijini kutembelea na kusimamia  miradi ya maendeleo ya Sekta mbalimbali inayoendelea kutekelezwa na mingine ipo katika hatua za ukamilishaji na kuweza kushauri na kushirikiana na Wananchi katika shughuli za ujenzi wa miradi husika na kuhakikisha inakamilika kwa wakati kwa kuzingatia ubora na viwango vya kitaalamu kwa  kufuata sheria, taratibu na kanuni na miradi itekelezwe na kukamilika  kulingana  na thamani ya fedha husika.

Mhe, Sweda amewataka Watendaji wote kutekeleza kikamilifu maelekezo na maagizo yanayotolewa na Viongozi wa Serikali na kuwakumbusha kuhusu maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt, John Pombe Joseph Magufuli na Makamu wa Rais Mhe, Samia Suluhu Hassan ya Wanancchi wote kufanya Usafi wa mazingira katika maeneo ya biashara na maofisini pamoja na kufanya Mazoezi ya Viungo kwa ajili ya kulinda afya na kujikinga na Magonjwa mbalimbali yasiyo ya kuambukiza , ambapo kila Mtumishi na Mwananchi anatakiwa kutekeleza maelekezo hayo kila Jumamosi ya pili pamoja na kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi,” nahitaji maelekezo hayo yaendelee kutekelezwa kwa kila Mkuu wa Idara na Vitengo kuwakumbusha Watumishi wake na Afisa Utumishi ahakikishe utekelezaji unafanyika katika Kata zote 27 kuanzia mwisho wa mwezi huu Septemba 2018 Watumishi wote wabadilike na kutimiza wajibu wao”.  Alisisitiza Mkuu wa Wilaya, Juma Sweda.

Awali, katika mazungumzo yake amezitaka Idara na Vitengo vya  Halmashauri kuwa na mpango madhubuti wa kutoa taarifa kwa Wananchi kupitia vyombo mbalimbali vya Habari kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa shughuli na miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kujengwa na iliyokamilika ili Wananchi waweze kuona namna Serikali ya awamu ya tano  inavyotekeleza na kuwapatia maendeleo ya  kiuchumi na kijamii.

Matangazo

  • Tangazo la Tozo za Ushuru na Leseni kwa Wafanyabiashara Wilayani Misungwi. September 17, 2018
  • Tangazo la Ajira mpya za Walimu wa Sekondari na Msingi na Shule walizopangwa kwenye Halmashauri July 16, 2018
  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili wa Nafasi ya Watendaji wa Kijiji Misungwi Tarehe 28/05/2018 May 21, 2018
  • Tangazo la Nafasi za Ajira za Mkataba katika Sekta ya Afya May 16, 2018
  • Angalia yote

Habari Mpya

  • Baraza la Madiwani laridhia na kupitisha Makisio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi ya Billioni 56.5 kwa mwaka 2019/2020 Misungwi.

    January 19, 2019
  • Madiwani Misungwi waridhishwa na kupongeza utekelezaji wa Miradi ya ujenzi kwa kutumia (FORCE AKAUNTI)

    October 30, 2018
  • DC Misungwi aagiza Mkataba wa Uchimbaji wa Madini ya Dhahabu wa Kikundi kupitiwa upya

    October 25, 2018
  • Kata ya Mondo yaibuka Kidedea yaongoza kwenye Sekta ya Kilimo na Elimu Wilayani

    October 09, 2018
  • Angalia yote

Video

Mkurugenzi Mtendaji Misungwi aagiza aliyetumbuliwa kwa vyeti feki akamatwe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Taarifa
  • Historia ya Halmashauri
  • Sheria Mbalimbali
  • Wasiliana Nasi
  • Malalamiko
  • Maeneo ya Uwekezaji
  • Huduma Sekta ya Afya

Viunganishi Linganishi

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tamisemi
  • Mwanza Region
  • Wakala wa Serikali Mtandao (Ega)

Ramani ya Wasomaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Misungwi

    Sanduku la Posta: P.O Box 20

    Simu ya Mezani: 255 732980745

    Simu ya Mkononi: 0763686106

    Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hatimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi . Haki zote zimehifadhiwa