• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ardhi na Maliasili
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Maeneo ya Vivutio vya Utalii
    • Maeneo ya Kilimo
    • Maeneo ya Madini
    • Maeneo ya Uwekezaji wa Mazingira
  • Huduma Zetu
    • Huduma Sekta ya Afya
    • Huduma Sekta ya Elimu
    • Huduma Sekta ya Maji
    • Huduma Sekta ya Mazingira
    • Huduma Sekta ya Maendeleo ya Jamii
    • Huduma Sekta ya Ardhi na Maliasili
  • Baraza la Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Huduma za Kijamii
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba Vikao vya Halmashauri
  • Miradi mbalimbali
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Mbalimbali
    • Taratibu
    • Gazeti la Serikali
    • Taarifa
    • Fomu mbalimbali
    • Zabuni
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Video Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Habari Mpya

Halmashauri Wilaya ya Misungwi yaadhimisha sherehe za miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania bara mwaka 2024 kwa kufanya usafi wa Mazingira.

Imewekwa : December 9th, 2024

Halmashauri Wilaya ya Misungwi yaadhimisha sherehe za miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania bara mwaka 2024 kwa kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya umma wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.

Akizungumza na Wananchi na Watumishi walioshiriki kufanya usafi katika maeneo ya Stendi ya Mabasi ya Misungwi, Soko kuu Misungwi pamoja na soko la jioni la Gwambina tarehe 9 Disemba 2024, Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Johari Samizi amewataka na kuwasihi wananchi kuendelea kufanya usafi katika maeneo yao na kudumisha amani, umoja na mshikamano wakati tukiadhimisha miaka 63 ya uhuru wa Tanganyika na kuwaonya wale watakaoendelea kupuuzia zoezi la usafi watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Mhe. Samizi ameongeza kuwa maendelo yaliyopatikana tangu kipindi cha Hayati Mwalimu Julius Nyerere hadi hivi sasa yametendeka mengi sana ikiwemo Daraja la JPM, Shule za msingi na Sekondari, miradi ya maji, Vituo vya afya na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya iliyopo Iteja,  pamoja na Barabara kupitia awamu ya sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuna mabadiliko sana ambapo asilimia kubwa ya watu ni vijana ambao hawakushiriki harakati za uhuru mwaka 1961, ila wana wajibu wa kuitunza ili kuikabidhi kwa vizazi vijavyo Taifa likiwa salama katika shughuli za kimaendeleo na fursa mbalimbali zipatikanazo katika awamu ya sita.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa  Halmashauri Wilaya ya Misungwi Bw. Addo Missama pia ametumia fursa hiyo kuwasihii wananchi kuendelea kutoa ushirikiano katika juhudi za kuhakikisha mazingira yanaendelea kuwa safi ambapo kila mmoja anapaswa kujenga utamaduni wa kuhakikisha eneo lake linakuwa safi muda wote kitendo ambacho kinapunguza atahari za kupata magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu. 

Naye Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Misungwi Bi. Elly Makala mara baada ya kushiriki shughuli za usafi amesema kuwa latika kuadhimisha miaka 63 ya uhuru Tanzania bara taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa wana jukumu la kuwashirikisha wananchi na kuwakumbusha kutoa ushirikiano katika kuzuia vitendo vya rushwa visitokee mapema ili kuwezesha kutekelezwa kwa miradi ya maendeleo kwa ubora na viwango vinavyotakiwa kulingana na thamani ya fedha.

Wakati huo huo Diwani wa Kata ya Misungwi  Mhe. Mganyizi Feruzi amesema kuwa ni jambo jema na la kupongeza kila mmoja kushiriki katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanzania bara ambapo amewasihi wananchi kutosubiri kuambiwa kuhusu usafi wa mazingira bvadala yake wafanye usafi kuwa sehemu yao ya maisha ili kuepuka magonjwa mbalimbali ya mlipuko ikiwemo kipindupindu. 

Baadhi ya Wananchi wa Misungwi akiwemo Bi. Mary Joseph na Bw. Abdalah Kisamba wameeleza namna ambavyo wameadhimisha siku ya uhuru  wamesema kuwa miaka 63 ya uhuru maendeleo yaliyopatikana kipindi cha Hayati Mwalimu Julius Nyerere hadi hivi sasa yametendeka mengi sana ikiwemo ujenzi wa Daraja la JPM la Kigongo hadi Busisi, ujenzi wa Reli ya kisasi ya SGR, Ujenzi wa Jengo la ofisi za Halmashauri ya Wilaya, Shule za msingi na Sekondari, Vituo vya afya na Hospitali ya Wilaya pamoja na Barabara kupitia awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuna mabadiliko sana tofauti na kipindi cha nyuma ambapo barabara zilikua chache huduma za afya na Elimu zilikua mbali na makazi, umeme na maji yalipatikana sehemu za miji pekee.

Wilaya ya Misungwi imeadhimisha Sherehe za Uhuru mwaka 2024 kwa kufanya usafi wa mazingira katika maeneo ya umma sambamba na kufanya Kongomano na mdahalo wa majadiliano ya Wananachi kuhusu maendeleo ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Ufundi na maendeleo ya jamii Misungwi, ambapo maadhmisho hayo yalipambwa na Kauli mbiu ya Miaka 63 “Uongozi madhubuti na ushirikishwaji wa Wananchi ni msingi wa Maendeleo yetu"




Matangazo

  • SHULE ZILIZOVUNJA REKODI KATIKA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2024 February 01, 2025
  • TANGAZO ZABUNI UPANGISHAJI VIBANDA VYA HALMASHAURI MWAKA 2023/2024 June 28, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 20, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE WA JIMBO LA MBARALI NA MADIWANI KATIKA KATA SITA ZA TANZANIA August 10, 2023
  • Angalia yote

Habari Mpya

  • DC Misungwi awataka Wananchi wa Kijiji cha Ibinza kata ya Isenengeja kudumisha amani na mshikamano.

    May 22, 2025
  • DC Misungwi akabidhi Vifaa saidizi vya Vitimwendo 15, Jezi na Mipira kwa Wanafunzi na Watoto wenye ulemavu kukwa Shule za msingi 16.

    May 21, 2025
  • Misungwi yapongeza kwa upatikanaji wa Mitambo ya kuondoa magugu maji itakayowasili mwishoni mwa mwezi julai 2025

    May 19, 2025
  • DC Misungwi awapongeza Waalimu wa Shule za Sekondari kwa ufaulu wa Asilimia 99.75

    May 16, 2025
  • Angalia yote

Video

Uzinduzi wa Tovuti za Mikoa pamoja na Halmashauri
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Takwimu za wanafunzi kitaifa
  • Taarifa
  • Kujisajili chama cha Mapinduzi-ccm
  • MFUMO WA UJAZAJI MATAMKO KWA NJIA YA MTANDAO
  • KUPATA KIUNGANISHI CHA MFUMO WA TAARIFA ZA SHULE-SIS
  • Historia ya Halmashauri
  • Sheria Mbalimbali
  • Wasiliana Nasi
  • Malalamiko

Viunganishi Linganishi

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tamisemi
  • Mwanza Region
  • Wakala wa Serikali Mtandao (Ega)

Ramani ya Wasomaji

world map hits counter

Wasomaji

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Misungwi

    Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI

    Simu ya Mezani: +255282983268

    Simu ya Mkononi: 0717259106

    Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.