Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Veronica Kessy amekagua na kuridhishwa na ujenzi wa Soko na Vibanda vya Wafanyabiashara linalojengwa katika Kata ya Usagara Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Veronica Kessy amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kuweka mazingira mazuri kwa Wafanyabiashara watakaokuwepo katika eneo la Soko pamoja na kuweka utaratibu wa Mikataba mizuri ya kisheria baina ya Mdau aliyejenga Soko sambamba na Wananchi waliojenga vibanda vya biashara kuzunguka eneo hilo la soko kwa malengo ya kufanya biashara.
Bi. Veronika Kessy amesema kwamba ni vyema Halmashauri ikaweka wazi utaratibu mzuri na kuingia mikataba na makubaliano ya muda na kikomo cha matumizi ya vibanda kwa Wafanyabiashara wote waliojenga ili kuondokana na migogoro na malalamiko yanayoweza kuibuka baadae, na kuzingatia gharama iliyotumika kujenga
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Usagara, Casmiry Zacharia Chai amesema kwamba Uongozi wa Kijiji cha Usagara kwa kuzingatia ushauri na maelekezo ya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi uliweka utaratibu kwa Wananchi tangu mwaka 2016 kwa Wananchi kuomba kujenga vibanda vya biashara ambapo Halmashauri iliweka gharama ya shilingi 150,000/= kwa ajili ya ramani na shilingi 20,000/= ikiwa ni gharama ya fomu ya maombi, ambapo awali viwanja vya mabdanda 74 vilivipimwa na baadae vibanda vingine viliongezeka ikiwa ni pamoja na eneo la ujenzi wa choo.
Bw. Csmiry Chai ameongeza kuwa hadi sasa vibada vilivyojengwa ni 109 na ujenzi umefikia hatua ya maboma na ujenzi unaendelea katika viwanja vilivyobaki ambapo Wafanyabishara wanajenga kwa gharama ya shilingi 6,500,000/= kwa kila kibanda kwa makadirio na ramani iliyotolewa na Idara ya Ujenzi.
Amesema kwamba katika ujenzi wa soko ambalo linajengwa na Mdau wa maendeleo kwa gharama zake na tayari jumla ya meza 270 zimeshatengenezwa kati ya meza 320 zinazotarajiwa kuwekwa katika eneo la soko na baada ya kukamilika utaratibu rasmi utaandaliwa kwa Wafanyabiashara kupanga na kufanya biashara kwa amani.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Bi. Leokadia Humera amesema kwamba Halmashauri awali iliandaa ramani na kuweka utaratibu wa Wafanyabaishara kujenga na mikakati iliyopo ni kuweka na kusaini mikataba ya kisheria kwa yoyote atakayekuwa amejenga vibanda na kupanga katika eneo la soko na kuweka makubaliano mazuri yatayofikiwa kwa manufaa ya pande zote kwa lengo la kujenga na kuleta maendeleo kwa Wananchi..
Mwonekano wa Soko lenye Meza 320 linaloendelea kujengwa katiika eneo la Mabanda ya Wafanyabiashara Kata ya Usagara Wilayani Misungwi ambapo Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Veronika Kessy ameagiza Halmashauri iweke utaratibu mzuri na kusimamia mikataba ya kisheria baina ya pande zote.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Bi. Veronika Kessy (katikati) akikagua na kutoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bi Leokadia Humera (Kushoto) akishuhudia na kupokea maelekezo ya Mkuu wa Wilaya ya Misungwi wakitoka katika eneo lililojengwa choo cha Soko na Vibanda vya Wafanyabiashara Kata ya Usagara na wengine ni wajumbe ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na Watendaji wa Halmashauri.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.