• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ardhi na Maliasili
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Maeneo ya Vivutio vya Utalii
    • Maeneo ya Kilimo
    • Maeneo ya Madini
    • Maeneo ya Uwekezaji wa Mazingira
  • Huduma Zetu
    • Huduma Sekta ya Afya
    • Huduma Sekta ya Elimu
    • Huduma Sekta ya Maji
    • Huduma Sekta ya Mazingira
    • Huduma Sekta ya Maendeleo ya Jamii
    • Huduma Sekta ya Ardhi na Maliasili
  • Baraza la Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Huduma za Kijamii
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba Vikao vya Halmashauri
  • Miradi mbalimbali
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Mbalimbali
    • Taratibu
    • Gazeti la Serikali
    • Taarifa
    • Fomu mbalimbali
    • Zabuni
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Video Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Habari Mpya

DC Misungwi aagiza TANROADS Mwanza kufanya Matengenezo ya haraka barabara ya Fullo -Nyambiti

Imewekwa : January 28th, 2020

Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda aagiza Wakala wa barabara Mkoani Mwanza, (TANROADS)  kuhakikisha wanafanya matengenezo ya dharula katika barabara ya Fullo – Nyabiti iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza.

Ametoa agizo hilo mapema leo baada ya kushuhudia na kuona hali halisi ya  ajali iliyotokea  ya Lori aina ya Fusso lenye namba T 704 DCD la  Sumve  lililokwama usiku wa tarehe 27 mwezi huu  katika daraja la Bujingwa- Kanyelele na kusababisha adha na kero kwa Wananchi na magari yanayopita katika barabara hiyo yakitokea Jiji la Mwanza kuelekea maeneo ya Sumve na Nyabiti Wilaya ya Kwimba.

“ Naitaka Wakala ya barabara Mkoa wafike na kuona namna miundombinu ya barabara ilivyo kwa sasa, pamoja na madaraja yameanza kubomoka kutokana na mvua hii inayoendelea na wachukue hatua kwa kufanya matengenezo haraka ili kunusuru na kuondokana na kero ya usafiri kwa Wananchi, abiria na magari ya mizigo”, alisisitiza Mkuu wa Wilaya  Sweda. 

Amewataka Wananchi Wilayani Misungwi kuchukua tahadhari hususani nyakati hizi za mvua wanapotumia barabara na kuwa wangalifu kwenye madaraja ya barabara hizo za vijijini ili kuepuka madhara na uharibifu  zaidi wa miundombinu  pamoja na kuwa watulivu na kuendelea kuchapa kazi kwa ajili ya kuleta maendeleo  na kujenga uchumi wao na taifa kwa ujumla.

Akizungumza kwa  njia ya simu Mwakilishi wa Meneja wa Wakala wa barabara (TANROADS) Mkoa wa Mwanza Mhandisi Joseph  Pius Mwami amesema kwamba tayari Wataalam wa uhandisi wameshafika katika maeneo ya barabara hiyo ya Fullo – Nyabiti na wamejiridhisha na kuona miundombinu ya barabara na madaraja yaliyoharibika katika barabara hiyo kutokana na mvua zinazoendelea na hatua za matengenezo zitaanza hivi karibuni.

Lori aina ya Fuso lenye namba T704 DCD lililokwama jana saa 12;00 jioni  katika daraja la barabara ya Fullo -Nyambiti ambalo lilikuwa likiendeshwa na dereva Deo Mathias Kachelwo wa Sumve, lori hilo lilisababisha adha kwa magari na Wasafiri wanaotumia barabara hiyo, hii ni kutokana na ubovu wa barabara unaosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Kisena Mabuba (kulia) wakiangalia na  kushuhuhudia namna Lori lililokuwa limebeba mizigo kutoka Mwanza baada ya kukwama katika daraja la Bujingwa -Kanyelele lilolopo kwenye barabara ya Fullo - Nyambiti inayopita Wilayani Misungwi, (katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Juma Sweda  akiwa pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya  akihakikisha usalama wa Wananchi na mali zao upo vizuri.

Mhandisi  Joseph Pius Mwami amesema kwamba Wakala imeshachukua hatua muda kwa kutoa Zabuni ya matengenezo na Mkandarasi  tayari ameshapatikana kwa ajili ya matengenezo ya barabara hiyo ya Fullo – Nyambiti yenye urefu wa kilomita 48, zitokazo meneo ya Bujingwa Wilayani Misungwi hadi Nyambiti Wilayani Kwimba.

Ameongeza kwamba tayari hatua za manunuzi kwa ajili ya matengenezo ya barabara hiyo zimeshafanyika na zitakapokamilika ujenzi utaanza mara moja na Wakala itahakikisha mataengenezo ya barabara hiyo yanafanyika kwa kiwango na ubora unaokubalika kwa mujibu wa taratibu na sheria.

Ametoa Wito kwa Wananchi kuwa wavumilivu hususani wakati huu wa mvua na kueleza kuwa Wakala itasimamia kikamilifu matengenezo hayo ili yaweze kukamilika kwa wakati na kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji wa mali na mizigo katika maeneo husika na kuwaomba kutoa ushirikiano wakati wote wa ujenzi.

Matangazo

  • SHULE ZILIZOVUNJA REKODI KATIKA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2024 February 01, 2025
  • TANGAZO ZABUNI UPANGISHAJI VIBANDA VYA HALMASHAURI MWAKA 2023/2024 June 28, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 20, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE WA JIMBO LA MBARALI NA MADIWANI KATIKA KATA SITA ZA TANZANIA August 10, 2023
  • Angalia yote

Habari Mpya

  • DC Misungwi awataka Wananchi wa Kijiji cha Ibinza kata ya Isenengeja kudumisha amani na mshikamano.

    May 22, 2025
  • DC Misungwi akabidhi Vifaa saidizi vya Vitimwendo 15, Jezi na Mipira kwa Wanafunzi na Watoto wenye ulemavu kukwa Shule za msingi 16.

    May 21, 2025
  • Misungwi yapongeza kwa upatikanaji wa Mitambo ya kuondoa magugu maji itakayowasili mwishoni mwa mwezi julai 2025

    May 19, 2025
  • DC Misungwi awapongeza Waalimu wa Shule za Sekondari kwa ufaulu wa Asilimia 99.75

    May 16, 2025
  • Angalia yote

Video

Uzinduzi wa Tovuti za Mikoa pamoja na Halmashauri
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Takwimu za wanafunzi kitaifa
  • Taarifa
  • Kujisajili chama cha Mapinduzi-ccm
  • MFUMO WA UJAZAJI MATAMKO KWA NJIA YA MTANDAO
  • KUPATA KIUNGANISHI CHA MFUMO WA TAARIFA ZA SHULE-SIS
  • Historia ya Halmashauri
  • Sheria Mbalimbali
  • Wasiliana Nasi
  • Malalamiko

Viunganishi Linganishi

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tamisemi
  • Mwanza Region
  • Wakala wa Serikali Mtandao (Ega)

Ramani ya Wasomaji

world map hits counter

Wasomaji

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Misungwi

    Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI

    Simu ya Mezani: +255282983268

    Simu ya Mkononi: 0717259106

    Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.