• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ardhi na Maliasili
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Maeneo ya Vivutio vya Utalii
    • Maeneo ya Kilimo
    • Maeneo ya Madini
    • Maeneo ya Uwekezaji wa Mazingira
  • Huduma Zetu
    • Huduma Sekta ya Afya
    • Huduma Sekta ya Elimu
    • Huduma Sekta ya Maji
    • Huduma Sekta ya Mazingira
    • Huduma Sekta ya Maendeleo ya Jamii
    • Huduma Sekta ya Ardhi na Maliasili
  • Baraza la Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Huduma za Kijamii
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba Vikao vya Halmashauri
  • Miradi mbalimbali
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Mbalimbali
    • Taratibu
    • Gazeti la Serikali
    • Taarifa
    • Fomu mbalimbali
    • Zabuni
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Video Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Habari Mpya

DAS Misungwi awataka Viongozi na Watendaji wa Serikali kuongeza ushirikiano na bidii katika Ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashuri.

Imewekwa : January 21st, 2025

Katibu Tawala Wilaya ya Misungwi Bw. Abdi Makange amewataka Viongozi na Watendaji wa Serikali kuongeza ushirikiano na bidii katika Ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashuri ili kukuza uchumi na kuimarisha shunguli za jamii wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.

Akizungumza wakati wa kikao maalum cha Kamati ya ushauri Wilaya tarehe 21 Januari 2025 Bw. Makange kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Johari Samizi amehimiza Viongozi na Watendaji wote kuendelea kusimamia na kukusanya mapato ya ndani ya Halmashauri ili kuweza kutimiza malengo yaliyowekwa kwenya Bajjeti za kila mwaka na amewapongeza wajumbe kwa ushiriki wao na kusisitiza kuwa mawazo yote yaliotolewa yatafanyiwa kazi ambapo ushirikiano thabiti unatakiwa kufanyika ili bajeti hiyo itekelezwe ikiwa ni pamoja na kuimarisha na kutekeleza kikamilifu miradi ya maendeleo.

Awali akiwasilisha rasimu ya Bajeti  ya mwaka 2025/2026 iliyokadiriwa shilingi Bilioni 53,614,834,111/= Afisa Mipango wa Halmashauri Bi. Peniel Titus amefafanua kwamba katika rasimu hiyo ya Bajeti kiasi cha shilingi 4,641,245,829/= ni fedha zitokanazo na vyanzo vya Mapato ya ndani ya Halmashauri ,kiasi cha shilingi. Bilioni 41,888,608,000/= ni fedha ya mishahara ya Watumishi, na kiasi cha shilingi Bilioni 1,359,841,000/= ikiwa ni  ruzuku ya uendeshaji ( OC) na kiasi cha shilingi Bilioni 5,725,139,282/= ni kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo na fedha zote ni kutoka Serikali kuu.

Bi. Peniel Titus ameeleza kuwa pamoja na kuwepo kwa rasimu ya bajeti hiyo ofisi ya Mipango na Uratibu imeahidi kutekeleza na kufanyia kazi mapendekezo na maadhimio ya kikao hicho kama ambavyo wajumbe wameshauri ikiwa ni pamoja na kuyapokea na kuyatekeleza ili kuhakikisha kuwa na maendeleo chanya katika jamii ndani ya Halmashauri ya Misungwi na kueleza kuwa makadirio ya Bajjeti hiyo yamelenga Zaidi kuongeza ustawi kwa jamii kupitia utekelezaji wa miradi ya maendelo na ukusanyaji wa Mapato ya ndani. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Misungwi Bw. Addo Missama kuwa kikao hicho ni maalum kwa ajili ya kupitia na kufanya tathmini ya utendaji kazi ambapo kwa  bajeti hiyo 2025/2026 atahakikisha inatekelezwa na kufanyiwa kazi akishirikiana na Wakuu wa Taasisi za umma, Wakuu wa Idara  na Vitengo vya Halmashauri ya Misungwi ili kutimiza malengo yaliyopangwa ili kufanikisha maadhimio na hatimaye kujiandaa na utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo katika Halmashauri.

Naye Meneja wa Wakala wa Barabara za mjini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Misungwi Mhandisi Kassim Shabani wakati akiwasilisha taarifa ya bajeti ya matengenezwwo ya Barabara amesema kuwa Misungwi ima mtandao wa barabara zilizosajiliwa na zenye urefu wa kilometa 927.54 km zilizogawanyika katika makundi na viwango vya lami,changarawe na udongo ambapo kwa mwaka wa fedha 2025/20226 TARURA inategemea kutengewa kiasi cha shilingi Bilioni 2,235,430,000/= kutoka Serikali kuu ambayo ni Tozo za mafuta, mfuko wa barabara na Mfuko wa Jimbo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wajumbe wa kikao hicho akiwemo Bi. Agness Kapingu ambaye ni  Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo TARI Ukiriguru amepongeza juhudi zinazofanywa na Halmashauri hiyo ambapo ametoa mapendekezo na kushauri kuhusu suala la utojia elimu endelevu kwa wakulima na wafugaji ili kukuza uelewa na kuwapa fursa zaidi katika sekta ya kilimo na uvuvi pamoja na Bw. Mussa Mwika ambaye ni Mwakilishi wa vyama vya siasa alishauri na kupendekeza kwamba Halmashauri iendelee kuweka mipango mizuri ya maendeleo ikiwemo kukamilisha ujenzi wa choo katika soko kuu la Misungwi na kutenga eneo la maegesho ya magari ili kuongeza mapato ya ndani.

Katika kikao hicho maalum cha Bajeti kilichowashirikisha wajumbe ambao ni pamoja na Viongozi wa Vyama vya siasa,Viongozi wa Dini, Wakuu wa Taasisi za umma, Wakuu wa Idara  na Vitengo vya Halmashauri ya Misungwi kwa ujumla wao walijadili na kutoa mapendekezo ya kina.




Matangazo

  • SHULE ZILIZOVUNJA REKODI KATIKA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2024 February 01, 2025
  • TANGAZO ZABUNI UPANGISHAJI VIBANDA VYA HALMASHAURI MWAKA 2023/2024 June 28, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 20, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE WA JIMBO LA MBARALI NA MADIWANI KATIKA KATA SITA ZA TANZANIA August 10, 2023
  • Angalia yote

Habari Mpya

  • DAS Misungwi awapongeza Watendaji Halmashauri kwa kushirikiana na Madiwani katika kuongeza ufanisi na ukusanyaji wa Mapato.

    April 29, 2025
  • Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi yafanya ziara ya yatembelea na kupata mafunzo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya nyang'hwale Mkoani Geita

    April 25, 2025
  • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango yaridhishwa na miradi ya maendeleo ya Halmashauri Wilaya ya Misungwi

    April 23, 2025
  • Kamati ya Lishe ya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi yawataka Watendaji wa Kata na Vijiji kutoa Elimu ya Shughuli za Lishe kwa Wananchi.

    February 27, 2025
  • Angalia yote

Video

Uzinduzi wa Tovuti za Mikoa pamoja na Halmashauri
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Takwimu za wanafunzi kitaifa
  • Taarifa
  • Kujisajili chama cha Mapinduzi-ccm
  • MFUMO WA UJAZAJI MATAMKO KWA NJIA YA MTANDAO
  • KUPATA KIUNGANISHI CHA MFUMO WA TAARIFA ZA SHULE-SIS
  • Historia ya Halmashauri
  • Sheria Mbalimbali
  • Wasiliana Nasi
  • Malalamiko

Viunganishi Linganishi

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tamisemi
  • Mwanza Region
  • Wakala wa Serikali Mtandao (Ega)

Ramani ya Wasomaji

world map hits counter

Wasomaji

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Misungwi

    Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI

    Simu ya Mezani: +255282983268

    Simu ya Mkononi: 0717259106

    Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.