Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Misungwi, Bw, Magange Mwita akitoa maelekezo kwa Waandikishaji wa Daftari la Wapiga kura (hawapo pichani) katika Mafunzo yaliyofanyika katika Ukumbi wa MGS Misungwi.
Baadhi ya Waandikishaji wa Daftari la Wapiga kura Willayani Misungwi wakifuatilia kwa makini maelekezo, kanuni na mwongozo wa Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019,mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa MGS Misungwi.
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Wilaya ya Misungwi, Bw, Alfonce Sebukoto akifafanua jambo kwa Waandikishaji wa Daftari la Wapiga kura Wilaya ya Misungwi kuhusu umuhimu wa kuzingatia kanuni, sheria na mwongozo katika zoezi la uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019
Afisa Uchaguzi Wilaya ya Misungwi, Bw, Dikson Kawovela akiwawezesha Waandikishaji wa Daftari la Wapiga kura Wilaya ya Misungwi kuhusu namna ya kufanikisha zoezi la uandikishaji wa Wapiga kura katika Vituo vilivyopo katika Vitongoji vyote 724 Wilayani Misungwi.
Baadhi ya Waandikishaji wa Daftari la Wapiga kura Wilaya ya Misungwi wakisikiliza na kufuatilia maelekezo kuhusu zoezi la Uandikishaji wa Wapiga kura katika Daftari kwa ajili ya Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019 kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Misungwi, Bw, Magange Mwita (hayupo Pichani).
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.