Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda akishiriki na Wananchi wa Tarafa ya Mbarika kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Wodi ya Wazazi (akina mama) inayojengwa kwa gharama ya shilingi 154,0000,000/= katika Kituo cha Afya Mbarika kwa ufadhili wa Shirika la Mama na Mtoto toka nchini Canada lilopo Wilayani Misungwi.
Mhe, Joel Dogani Diwani wa Kata ya Mbarika akishirikiana na Wananchi wa Tarafa ya Mbarika kwenye uzinduzi wa uchimbaji wa msingi wa ujenzi wa Wodi ya Wazazi inayojengwa katika Kituo cha Afya Mbarika,ambayo itakuwa na Vitanda 24 na itahudumia Wakazi zaidi ya 58,000 wa Tarafa ya Mbarika.
Mhe, Joel Dogani Diwani wa Kata ya Mbarika (kushoto) akizungumza na Wananchi kuhusu ushiriki wa jamii katika ujenzi wa Wodi ya Wazazi na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda (kulia ) pamoja na Kisena Mabuba Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, wakisikiliza wakati wa zoezi la uzinduzi wa Ujenzi wa Wodi ya Wazazi Kituo cha Afya Mbarika.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda pamoja na Wananchi wa Mbarika wakishiriki pamoja kuchimba msingi wa ujenzi wa Jengo la Wodi ya Wazazi inayojengwa katika Kituo cha Afya Mbarika.
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mbarika wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Juma Sweda alipotembelea katika Sekondari hiyo kukagua na kuzindua vyumba 2 vya madarasa vilivyokamilishwa kwa gharama ya shilingi 25,000,000 pamoja na madawati 80 kwa ufadhili wa fedha za Serikali na kuwasihi waongeze bidii katika masomo na kufaulu kwa manufaa yao na taifa zima.
Mhe, Juma Sweda Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, akisisitiza kuhusu Wanafunzi kupenda masomo na kuachana na tabia mbaya na uzembe wakati wakiwa shuleni ili kuongeza ufaulu na kuinua kiwango cha Elimu hapa nchini na kuwataka kusoma zaidi kutokana na fursa ya Madarasa na Walimu wazuri walionao kwa sasa, wakati akizungumza na Wanafunzi (hawapo pichani) na Walimu wa Sekondari ya Mbarika.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.